mwanazuoni

MASHINDANO YA CHUACHUA CUP YAANZA KWA KISHINDO KIKUBWA MASASI



Jana mnamo majira ya sa 10:36 jioni katika uwanja wa mpira maarufu Bomani, palifanyika uzinduzi wa mashindano ya Chuachua Cup.
mashindano hayo yanajumuisha timu 20. Timu 14 ni za mpira wa miguu kwa wanaume na timu 6 za mpira wa miguu kwa wanawake.

katika uzinduzi huo wa jana uliambatana na mechi kali na ya kukata na shoka kati ya wenyeji timu ya MAENDELEO VS MAKURANI.

MATOKEO
 MAENDELEO 2  - 3 MAKURANI

Goli la kwanza la timu ya Makurani liliwekwa nyavuni dakika 17 ya mchezo, dakika ya 24 Hamisi Ally aifungia timu yake ya Makurani goli la pili lililodumu mpaka mapumziko. hivyo mpaka mapumziko MAKURANI 2 - 0 MAENDELEO.
 Kipindi cha pili cha mchezo mpira ulikuwa wa kasi na kushambuliana kwa timu zote mbili. Dakika ya 53 Makurani waliweza kupata goli la 3 kupitia mshambuliaji wao.

Dakika ya 60 ya mchezo timu ya Maendeleo iliamka kutoka usingizini kama ndovu aliyejeruliwa na kuandika bao la kwanza kuptia mchezaji wao Atanas, na dakika ya 63 timu ya maendeleo iliandika goli la pili kupitia winga wao Tariq.

Mpaka kipenga cha mwisho cha Mwamuzi wa mchezo huu matokeo ni 
MAENDELEO 2 - 3 MAKURANI.




Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment