mwanazuoni

Kamati ya JPM na Barrick Gold zimekutana kujadili uchimbaji Madini

Majadiliano kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais Magufuli na Wawakilishi kutoka Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo hapa nchini yameanza leo July 31, 2017 Dar es Salaam.
Kamati hiyo inaongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi wakati Kamati ya Barrick Gold Corporation inaongozwa na Afisa Mwendeshaji Mkuu Richard Williams.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa majadiliano hayo Prof. Kabudi amesema Kamati yake imejipanga vizuri kujadiliana na Barrick Gold Corporation juu ya madai ya Tanzania  katika biashara ya madini na itahakikisha inasimamia maslahi ya Tanzania ipasavyo.
Naye Richard Williams ameshukuru kuwepo kwa majadiliano hayo akisema Kampuni ya Barrick Gold Corporation imeyapokea madai ya Tanzania  kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye maslahi kwa pande zote mbili.


Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment