mwanazuoni

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA MPO WAPI ?

Napenda kuchukuwa nafasi kuelekeza kilio changu kwa taasisi inayoshughulikia haki za binadamu nchini Tanzania kwani wameshindwa kutenda haki au wamesahahu majukumu yao. 

Ifahamike kuwa miongoni mwa haki za kijamii  kwa mujibu wa  Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (“The International Covenant on Economic, Social and Cultural Rights”,  ICESCR ) wa 1966 ni pamoja na haki ya kupata maji safi na salama.


Hata hivyo  katika nchi yetu  inaonekana haki ya kupata maji safi na salama haitiliwi mkazo pamoja na Tanzania kutambua na kuridhia mkataba huo hivyo malalamiko haya ya lengo la kuwezesha tume kusimamia haki za msingi za binadamu na utawala bora katika sekta ya maji.
Ikumbukwe  kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, toleo la mwaka 2005 Ibara ya 130 (b)  na (c) inaeleza majukumu ya Tume ya Haki za binadamu na utawala bora kuwa ni pamoja na kupokea malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu  na kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa utawala bora;
Izingatiwe kuwa Sheria ya Haki za binadamu na Utawala Bora  namba  7 ya mwaka 2001 kifungu cha 22(1) kinaruhusu malalamiko kwa njia ya maandishi ;
Na Irejewe kuwa kuwa kifungu cha 15(1) (b) (iii)  cha Sheria ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, sheria namba 7 ya mwaka 2001, kinaipa nguvu Tume kuchunguza uvunjaji wa Haki za Binadamu  ikiwa itapokea malalamiko kutoka kwa mtu anayefanya hivyo kwa niaba ya kundi la watu.

Hivyo basi tunaomba tume ya haki za binadamu na utawala bora ichukue hatua za makusudi kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanaishi na kupata haki ya kupata maji safi na salama.

Pia kilio changu nakipelekea kwa wananchi na wakazi wa Morogoro kumchangua kiongozi ambaye hana masilah na wananchi wake hasa Diwani wa Kihonda kushindwa kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata maji safi na salaama ila awali ya yote Tume za haki za binadamu na utawala bora mna dhima hii ya kuhakikisha kuwa wakazi wa kihonda wanaishi kama binadamu wengine , kitendo cha kukosa maji safi na salama ni dalili kuwa hawana haki ya kuishi japo kuwa wao ni watanzania kama wengine na wanalipa kodi bila kuangalia kama wanapata huduma hiyo.

Ni ajabu kuona karne ya 21 watu wanaishi kama wapo karne ya 5, hata wanyama wenyewe hawapo hivyo. hivi kweli tume ya haki za binadamu na utawala bora nma fanyakazi zenu ?


                   

             
 
 
 
 
 
 
Ebu tazama baadhi ya hizo picha huone jinsi gani watu wanavyopata tabu ya maji safi na salama wakati wewe umekaa ofisini kazi kupiga story na kuacha majukumu yako.


MSHANA JUNIOR ( ACTIVIST)
31 OCTOBER 2012
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment