HALI YA SINTOFAHAMU YAIKUMBA SHULE YA SEKONDARI MANZESE
Pichani ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Manzese iliyopo jijini Dar es salaam maeneo ya Uzuri. Leo majira ya asubuhi ilitokea hali ya kustajabisha kwa kuwa wanafunzi walikuwa wanakimbia hovyo na wengine kuanguka bila kujulikana kupatwa na tatizo gani, ila wajuzi wa mambo wanasibisha na NGUVU ZA GIZA.Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.
Chanzo chetu cha habari kinaendela kufatilia ili kujua nini hasa kiliwakumba wanafunzi hao.
0 comments:
Post a Comment