mwanazuoni

WEMA SEPETU YAMKUTA MAKUBWA





MISS Tanzania 2006 ambaye pia ni mcheza filamu mkali Bongo, Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alikumbwa na kizaazaa cha kutaka kutekwa na watu wasiojulikana wakimtuhumu kuwatukana kupitia Facebook.
 
Mrembo Wema Isaac Sepetu.
Akizungumza na Amani jijini Dar juzi, Wema alisema tukio hilo lilimtokea Kijitonyama, Dar wakati akitoka kwenye mishemishe zake kuelekea nyumbani kwake.
Alisema alipofika maeneo hayo, gari asilolijua lilimpita na kwenda kusimama mbele yake kisha wakashuka watu asiowajua na kuanza kumuuliza ni kwa nini anawatukana katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
“Nilivyosikia wanasema Facebook, roho yangu ikatulia maana najua kuna watu kama 37 wanaotumia jina langu na picha zangu kwenye Facebook, nilishuka kweye gari na kuanza kuwaelewesha kuhusu hilo, bahati nzuri walinielewa,” alisema Wema.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment