Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu alisema Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Zanzibar ilikutana mwishoni mwa wiki na ilipendekeza majina mawili likiwamo hilo la Mattar na kuwasilisha kwa Kamati Kuu ya CCM.
Kamati kuu ya halmashahuri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi kimeteua na kupitisha jina la Mattar Saharan Said kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Chambani, wilaya ya mkoa, mkoa wa kusini Pemba.
Uchaguzi wa jimbo hilo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge, Salim Hemed Khamis (CUF) aliyefariki Machi 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati akihudhuria moja ya vikao vya Kamati za Bunge.
Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
Zanzibar, Waride Bakari Jabu alisema Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM Zanzibar ilikutana mwishoni mwa wiki na ilipendekeza
majina mawili likiwamo hilo la Mattar na kuwasilisha kwa Kamati Kuu ya
CCM.
Kamati hiyo ilipitisha uteuzi huo katika kikao
chake cha siku moja kilichofanyika mjini Dodoma jana chini ya Mwenyekiti
wake, Rais Jakaya Kikwete.
Katika kikao hicho, pia imemteua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Idd kuzindua kampeni hizo,
Mei 18 mwaka huu wakati naye Mwenyekiti mstaafu wa
CCM na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi atafunga
kampeni hizo kabla ya uchaguzi Juni 6.
CHANZO: GAZETI LA MWANANCHI 16/05/2013
CHANZO: GAZETI LA MWANANCHI 16/05/2013
0 comments:
Post a Comment