Katika
tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa
mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya
kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu
wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana na
Katibu Mkuu wa CDM Ndugu Slaa.
Kutokana na hudhuri wa Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri kuelekea Dodoma kwenda
kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa na majukumu mengine
muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na Uenezi
CCM, ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi wa
vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi
yetu.
Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni
asubuhi ya Leo, Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa
atamuwakilisha Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya
kusikia kauli hiyo, Dr Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi
kuongea na Nape kwa sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake.
Hata
busara zilipotumika za kumsihi apungumze munkari na kumtaka kuangalia
umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa watanzania, bado Slaa
aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV.
Baada ya tahamaki
hiyo, mijadala ya pembeni ya mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa
kimsingi Slaa anamuogopa Nape katika mijadala ya kisiasa, nahii ni
kutokana na uwezo wa Nape katika kujenga hoja na kuzilinda na kuzitetea
hoja hizo...
Tukio hilo linadhihirisha kukosa uvumilivu wa
kisiasa (lack of political tolerance) ambako viongozi wa CDM hasa Slaa
wanao..... Hii ni kwa sababu Nape alimtaka aeleze ni kusemwa vibaya kupi
ambako yeye Slaa anakumaanisha na akashindwa kubainisha.....
Hali
hiyo pia imeonesha taswira ya political immaturity kuwa viongozi wa aina
hii hawajakomaa ...
Pia,
tukio hilo linaweka wazi kuwa CDM hawako tayari kuyazungumzia ana kwa
ana matatizo yaliyotokana na Siasa mbovu za matusi....
Tabia hii ya kukwepa kuyashughulikia makosa ya kisiasa kutalileta Taifa letu madhara makubwa sana. ...kukataa kulikubali tatizo tulilonao la siasa mbofu zenye kuhamasisha chuki, utengano, udini, ukabila na hata kuendesha matukio ya kudhuru watu na mauaji ni makosa.
Mtani
Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
0 comments:
Post a Comment