mwanazuoni

HOTUBA YA RAIS WA TANZANIA YA MWEZI WA SABA


Utangulizi
Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi
Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha
kwa mara nyingine tena kutekeleza utaratibu wetu huu mzuri
tuliojiwekea wa Rais kuzungumza na taifa kila  mwisho wa
mwezi.
Mwezi Julai, 2013 ulikuwa wa neema kubwa ya wageni kwa
nchi yetu wakiwemo watu na viongozi mashuhuri duniani.
Natoa shukrani nyingi kwa Watanzania wenzangu kwa jinsi
tulivyowapokea wageni wetu zaidi ya 1,700. Wamefurahi
kuwepo kwao nchini na wameondoka wakiwa na kumbukumbu
nzuri ya nchi yetu.  Wageni wetu wamekuwa wa manufaa
makubwa kwa nchi yetu.  Wamesaidia kuitangaza Tanzania
duniani na kuendeleza fursa za kukuza utalii, biashara na
uwekezaji nchini na kwingineko katika Afrika.
Mkutano wa Smart Partnership
Wageni wetu wa kwanza ni wale waliokuja kuhudhuria
Mkutano wa
uliofanyika Dar es Salaam tarehe 28 Juni hadi 1 Julai,
2013.  Mkutano huo
ulihudhuriwa na watu zaidi ya 800 kutoka mabara yote duniani
wakiwemo Watanzania.  Miongoni mwa waliohudhuria ni
pamoja na wakuu wa nchi na Serikali, viongozi wastaafu,
wanadiplomasia, wawakilishi wa mashirika na taasisi za
kimataifa, makampuni ya ndani na nje, wafanyabiashara,
wasomi, asasi za kijamii na watu wa makundi mbalimbali katika
jamii.  Makampuni yetu 21 nayo yaliungana na makampuni
mengine 28 kutoka nje ya nchi kushiriki kwenye maonesho ya
matumizi ya sayansi na teknolojia yaliyofanyika sambamba na
mkutano huo .
Agenda kuu ya majadiliano ya mwaka huu ilikuwa ni
“ Matumizi ya teknolojia kama nyenzo ya kuleta
maendeleo ya kijamii na kiuchumi Barani
Afrika (
).
Tuliichagua mada hii kwa kuwa ni ukweli ulio wazi kuwa
matumizi ya sayansi na teknolojia ndiyo chachu
kubwa iliyoleta mageuzi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii
katika nchi. Ndiyo siri ya mafanikio katika nchi zilizoendelea na
zinazopiga kasi kubwa ya maendeleo duniani.
Bahati mbaya sana kumekuwa na maendeleo na matumizi
madogo ya sayansi na teknolojia katika Afrika.  Ndiyo maana
nchi za Afrika ziko nyuma kimaendeleo ukilinganisha na zile
zilizoendelea.  Katika mkutano huo umuhimu wa kuendeleza
na kuongeza matumizi ya sayansi na teknolojia kwa ajili ya
maendeleo Barani Afrika ulitambuliwa na kusisitizwa.
Mkutano ulihimiza na kusisitiza kuwa sera, mikakati na
mipango ya maendeleo ya nchi za Afrika zitoe kipaumbele kwa
kuendeleza matumizi ya sayansi na teknolojia.  Nchi zetu
zimehimizwa kuwekeza katika elimu ya sayansi na teknolojia
pamoja na kujenga uwezo wetu wa ndani wa uvumbuzi,
ubunifu, umiliki na uendelezaji wa sayansi na teknolojia. Aidha,
imesisitizwa kwa nchi zetu ziongeze  kasi ya kutumia sayansi
na teknolojia katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii
ili kuongeza ufanisi na kasi ya maendeleo.
Jambo la kutia faraja kwetu nchini ni kwamba mambo yote
hayo tunayafanya.   Tunachotakiwa sasa ni kufanya vizuri zaidi
na kuongeza uwekezaji na kasi ya kuendeleza matumizi ya
sayansi na teknolojia katika shughuli za maendeleo ya
kiuchumi na kijamii nchini.  Tutaendelea kuboresha sera,
kuboresha mazingira ya uwekezaji na kwa ajili ya maendeleo
ya sayansi na teknolojia nchini.
Ziara ya Rais wa Marekani Nchini Tanzania
Mgeni wetu wa pili alikuwa Rais wa Marekani, Mheshimiwa
Barack Obama, aliyefanya ziara nchini kwetu kati ya tarehe 1  -
2 Julai, 2013.  Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano
wa kihistoria uliopo kati ya Marekani na Tanzania.  Kama
mjuavyo, nchi zetu mbili zina uhusiano wa kibalozi tangu Uhuru
wa Tanganyika mwaka 1961 na Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar mwaka 1964.
Uhusiano wetu umepita katika vipindi mbalimbali na kwamba
hivi sasa umekuwa mzuri zaidi kuliko wakati mwingine wowote
katika historia ya nchi zetu mbili.  Kumekuwepo na ongezeko
kubwa la misaada ya maendeleo kutoka Marekani na
uwekezaji wa vitega uchumi na biashara navyo vinakua. Pia
ziara za kiserikali za viongozi wa nchi zetu kutembeleana
zimeongezeka. Kama mtakavyokumbuka, mwaka 2008
aliyekuwa Rais wa Marekani Mheshimiwa George W. Bush
alifanya ziara ya siku nne nchini.  Pia Mawaziri mbalimbali wa
Serikali ya Marekani wametembelea Tanzania akiwemo
Mheshimiwa Hilary Clinton akiwa Waziri w
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment