Mh. Dkt. Kigwangala, Naibu Waziri hebu tujuze;
1. Je kabla ya mtoto Getrude Clement kwenda kuhutubia Umoja wa Mataifa ulikuwa unamjua? Wizara yako ilikuwa inamtambua?
2. Je ulienda kumuaga kabla hajaenda? Ulikuwa unajua anaenda? Au ndio
tabia zile zile za kutambua mchango wa mtu baada ya kufa? Wewe umetambua
uwezo wake baada ya kurudi!! 3. Je umejua lini kwamba baba yake ni
kinyozi na mama yake ni mfanyabishara ndogo ndogo?
4. Sasa kwa nini Foundation yako ndio itamlipia ada ya Form 5 na 6 badala ya Wizara yako?
5. Unasema utampeleka shule ya kisasa kwani mbona kwenye shule ya kata
aliyosoma amefikia hapa ulipomkuta? Unadhani kwa nini asiendelee shule
ya kata? Wengine waendelee huko kwa nini?
6. Je huyu ni mtoto
pekee mwenye kipaji? Wizara yako ina utaratibu gani kuwatambua na
kuwaendeleza watoto wenye vipaji? Au ndio Foundation yako itafanya?
7. Hujasema lolote kuwapongeza wazazi wala kuwatia moyo wazazi wengine. Huoni mchango wa wazazi?
Tuache kufanya maamuzi kwa matukio. Hakuna sustainability wala matokeo
yenye tija. Ndio maana inaweza kuonekana ni maigizo au kutafuta
political mileage.
Tunategemea taarifa rasmi inayojitosheleza
kutoka Wizara yako na sio post FB au kwenye social media. Watoto wako
wengi. Huyu sio wa kwanza au wa mwisho.
Hongera sana Getrude Clement pamoja na Wazazi wako, Walimu wako na wote waliokusaidia kufikia hapa. Mungu akubariki.
Home / habari /
matukio /
siasa
/ MASWALI SABA MAZITO YA MSANDO ALBERTO KWA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII , JINSIA, WAZEE NA WATOTO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment