mwanazuoni

MTOTO MCHANGA ATOLEWA KWENYE VIFUSI NAIROBI

mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka siku ya Ijumaa jijini Nairobi nchini Kenya.
Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.
Akizungumzia hali ya afya ya mtoto huyo, Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai amesema kuwa hali ya mtoto huyo inaendelea kuimalika tangu alipofikishwa hospitalini jana.Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini.
Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo.


Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment