NAIBU BALOZI WA UINGEREZA AISIFU TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE
NAIBU balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, ameisifu
taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa
moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa.
Pongezi hizo amezitoa leo baada ya kutembelea kambi
hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo na kujionea madaktari wakiendelea na kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Taasisi ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake
nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na vifaa, ambao wanashirikiana na madaktari na wataalamu wengine kutoka JKCI na kufanya upasuaji wa watoto 20 hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment