mwanazuoni

Obama: Clinton anafaa zaidi kuongoza Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama amemsifu sana mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton na kusema ndiye afaaye zaidi kuongoza Marekani.
Akihutubia katika kongamano kuu la chama cha Democratic mjini Philadelphia, huku akishangiliwa na wajumbe, Rais Obama amesema hakujawahi kuwa na mtu aliyehitimu zaidi kuongoza Marekani kuliko Bi Clinton.
“Hakujawahi kuwa na mwanamume au mwanamke, iwe mimi au Bill Clinton au mtu mwingine yeyote aliyekuwa amehitimu zaidi kuwa rais kama yeye,” amesema Bw Obama.
Amemsifu pia kwa kujikakamua na kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya taifa hilo kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama kikubwa.
Amempongeza kwa kubomoa vizuizi na kuunda nafasi zaidi kwa Wamarekani.
Amewaahidi Wamarekani kwamba Bi Clinton anatetea umoja na maadili ya Wamarekani.
Bw Obama pia amemkosoa vikali mgombea wa chama cha Republican Donald Trump.
Awali, Seneta wa Virginia Tim Kaine alikubali rais uteuzi wa kuwa mgombea mwenza wa Bi Clinton.
Source: BBC
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment