mwanazuoni

Mamia waandamana kupinga ufisadi serikalini Kenya



Mamia ya watu wamekusanyika eneo la Freedom Corner katika Uwanja wa Uhuru Park, katikati mwa jiji la Nairobi, kuandamana kulalamikia wanachosema ni ongezeko la visa vya ufisadi serikalini. Maandamano hayo yanafanyika siku chache baada ya gazeti moja kuchapisha habari zinazodai jumla ya dola 50 milioni za Marekani katika wizara ya afya zilitumiwa vibaya au zikaporwa.
Serikali imekanusha madai hayo.
Wanaharakati walioandaa maandamano ya leo wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta achukue hatua la sivyo ajiuzulu.
Polisi wametumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya.

Polisi wa kupambana na fujo wakiwa uwanja wa Uhuru Park
Image captionPolisi wa kupambana na fujo wakiwa uwanja wa Uhuru Park
Baadhi ya waandamanaji wamejifunga minyororo mikononi
Image captionBaadhi ya waandamanaji wamejifunga minyororo mikononi
Rais Uhuru komesha ufisadi au jiuzulu, yanasema baadhi ya mabango
Image captionRais Uhuru komesha ufisadi au jiuzulu, yanasema baadhi ya mabango
Maandamano Nairobi
Chanzo:bbc

Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment