mwanazuoni

Mafuta ya kupanga uzazi kwa wanaume yafaulu majaribio



Mafuta yanayotumiwa na wanaume katika mpango wa uzazi yamefaulu, baada ya kufanyiwa majaribio kwa tumbili.
Majaribio ya mafuta hayo mapya yanayozuia mbegu za kiume kuingia kwa pamoja na mafuta hayo, yamefanyiwa majaribio kwa tumbili na kuonekana kufaulu.
Mafuta hayo yaitwayo Vasalgel, yanatumika kama kizuizi, mara inapodungwa ndani ya mishipa ya kupitishia mbegu za kiume kwenye uume wa mwanamume.

Mpango wa uzazi kwa wanaume

Ukataji wa mshipa wa kupitishia mbegu ya kiume ya uzazi, huwa ni tendo la kudumu, licha ya kuwepo kwa wanaume ambao hufanyiwa operesheni ya kurejesha tena hali hiyo

  Kampuni inayoshughulikia hilo, inasema kuwa majaribio hayo yaliyodumu miaka miwili iliyopita, na kuchapishwa katika jarida la Basic and Clinical Andrology, yanaonyesha kuwa kuwa mafuta hayo yanafanya kazi na ni salama kwa wanyama wanaofanana na binadamu.

 

Inaleta matumaini kuwa na ushahidi tosha, kuanza kufanyiwa majaribio kwa wanaume wa kibinadamu katika kipindi cha miaka michache ijayo.
Ikiwa mradi huo utapata fedha za msaada, bila shaka utawasaidia wanaume wengi duniani kujumuika ipasavyo katika hali ya mpango wa uzazi.bbc
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment