Milipuko imesikika katika mji Mkuu wa Mogadishu nchini Somalia usiku wa kuamkia leo.
Kumekuwa
na taarifa kuwa mizinga imelipuliwa karibu na uwanja wa ndege ambapo
uchaguzi unatarajiwa kufanyika, huku wakazi wa eneo la Waberi iliyoko
Kusini Magharibi mwa Mogadishu pia wakithibitisha kusikia milipuko.
Kufikia
sasa hakuna maafa au majeruhi walioripotiwa ingawa hali ya wasiwasi
imetanda Mogadishu. Babarabara zote zimefungwa. Uwanja wa ndege
hakuendeki. Na hata wakaaji wengine hawawezi kuvuka kutoka barabara hii
hadi ile.
Mahali pa kufanyia uchaguzi pamehamishwa, kutoka Chuo
cha Polisi hadi Uwanja wa ndege wa Mogadishu wenye ulinzi mkali. Sababu
ya kuongezeka kwa vitisho vya usalama na rushwa .
Hii leo Ndege hazitaruhusiwa kutua au kupaa kutokea uwanja huu, kwa kuwa ni siku ya kupiga kura.
Mfumo
wa uchaguzi nchini Somalia umeharibika kama ilivyo miundombinu yake.
Haina daftari la wapiga kura. Wabunge mia tatu na ishirini na tisa ndio
watakaomchagua Rais ajaye. Lakini sasa tuhuma za rushwa zinatishia
kuvuruga mchakato mzima. Kuna tuhuma nzito kuwa wabunge wengi wamelipwa
mamilioni ya dola kushawishi upiga-kura wao.
Wanawake wengi zaidi watashiriki kupiga kura wakati huu, hivyo
kufanya asilimia ishirini na sita ya kura zote za bunge. Ingawa wanawake
wawili waliotangaza nia ya kuwania Urais akiwemo Fatuma Dayyib
aliyetangazwa sana, walijitoa.
Licha ya maswali mengi kuhusu
uchaguzi huu, wananchi wa Somalia wanatumai kuwa kufanikiwa kwa uchaguzi
huu utawaongoza kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020. Lakini kwanza, nchi
inahitaji Rais na serikali inayofanya kazi.bbc
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment