mwanazuoni

Chama cha wafanyikazi chamtaka Zuma kujiuzulu

Chama kikubwa cha wafanyikazi nchini Afrika Kusini, Cosatu kimeunga mkono kauli ya wale wanaomtaka rais Jacob Zuma kujiuzulu.
Japo Cosatu kinajulikana kuunga mkono chama tawala ANC, kimemshutumu rais Zuma kwa kile wanachokitaja kuwa na uhusiano wa karibu mno na familia moja ya jamii ya Wahindi huko Afrika Kusini, waitwao Gupta, wanaodaiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika serikali ya Zuma.
Bw. Zuma na falimia hiyo ya Guptas, wamekana kufanya kosa lolote.
Wiki iliyopita chama chengine mshirika wa ANC The South African communist party pia kilimtaka Bw. Zuma kung'atuka mamlakani kutokana na kashfa tele zinazozidi kumuandama, madai ya makosa ya ufisadi.
Sarafu ya Rand imekuwa ukiyumba yumba kutokana na malumbano hayo ya kisiasa nchini Afrika Kusini hasa tangu kufutwa kazi kwa aliyekuwa waziri wa fedha nchini humo Pravin Gordhan.bbc
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment