mwanazuoni

UTAFITI: Naambiwa imegundulika dawa ya kuzuia usizeeke na inatibu kisukari

April 2 2017 nimekutana na stori ambayo inawahusu wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha New South Wales Marekani kugundua dawa zitakazomzuia mtu kuzeeka, huku zikisaidia kurekebisha seli za mtu aliyezeeka na kurekebisha vinasaba ‘DNA’ vilivyoharibika ambavyo ndio sababu kuu ya uzee.
Mkuu wa utafiti huo Professor David Sinclair aliiambia Science Today kuwa: >>>”Dawa hizi zitazuia uzee kwa kupambana na magonjwa yote yanayosababisha ngozi na mifupa ya binadamu kuharikibika. Itaponya magonjwa kama Kisukari, Saratani na magonjwa mengine yanayosababishwa na uzee, pia itasaidia kulinda kiwango cha mafuta mwilini ‘Calories’ na kuongeza maisha marefu”
Ripoti ya utafiti huo ilionesha jaribio la kwanza lilifanywa kwa panya mzee ambapo baada ya wiki moja kulikuwa na mabadiliko chanya kwenye ngozi na seli zake zikionekana kuimarika kwa kiasi kikubwa, huku jaribio la kwanza kwa binadamu linatarajia kufanywa mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo ndani ya miaka mitano dawa hizi zitaanza kupatikana madukani dunia nzima.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment