mwanazuoni

MWIGULU AWE KATIBU MKUU YANGA


Kutokana hali ya mambo ilivyo. Usalama wa wananchi ukiwa mdogo nchini. Watu wanapotea na taarifa sahihi hazipatikani.
Kutokana na kuzingatia kuwa dhamana ya kusimamia usalama wa raia na mali zao, imekabidhiwa kwa Jeshi la Polisi, chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Na kutokana na kufahamu kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani, ipo chini ya Waziri Mwigulu Nchemba.
Kwa kuwa suala la kupotea Roma na wenzake mpaka sasa haijulikani hatma yake. Vilevile ikiwa ni miezi sita sasa tangu Ben Saanane alipotoweka.
Kwa kukumbuka matukio ya uvamizi Clouds TV, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kutishiwa bastola. Wasanii kukamatwa bila mpango na hata kuachiwa kwa agizo la Rais Magufuli, wakati Mwigulu kama waziri mwenye dhamana akiwa hajatoa majibu yenye kuridhisha.
Kwa kukumbuka pia watu kuitwa wauza unga bila ushahidi, yeye kubaki kimya. Huku pia ikidaiwa kuwepo kwa viongozi walioghushi vyeti ambalo ni kosa la jinai, hilo pia akawa kimya.
Kwa kuwa pia hatujasahau kuhusu miili ya watu waliokutwa wametupwa Mto Ruvu, ikiwa imepita miezi mitano bila kupewa majibu ya watu hao.
Vilevile, kwa kutambua kuwa Waziri Mwigulu amekuwa mwepesi sana kushughulika na masuala ya Klabu ya Yanga, anayoipenda sana kuliko majukumu ya kuhudumia wananchi wote kiserikali ambayo anayo.
Nashauri ya kwamba ni vema Mwigulu awe tu Katibu Mkuu Yanga au cheo kingine Yanga, bila shaka huko atawajibika vizuri zaidi. Hili la Wizara ya Mambo ya Ndani, tafadhali sana, Rais Magufuli angeteua mwingine ambaye atakuwa macho na majukumu yake kuliko sasa na Mwigulu.
Ndimi Luqman MALOTO
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment