mwanazuoni

Ushindi usio rahisi wa Mancity dhidi ya Donetsk

Mabingwa wa Ukrain Shakhtar walidhihirisha kuwa timu bora kuwahi kupambana na City msimu huu na mabingwa hao walikabiliwana kibarua kigumu kabla ya ya kufanikiwa kukusanya pointi tatu.
City walitarajiwa kuwanyorosha wapinzani wao lakini walighdhabishwa kwa ufunguzi wa kipindi cha kwanza bila ya kufunga bao.
Kevin de Bruyne alifunga goli lake safi la kwanza la msimu baada ya kubadilishana pasi na David Silva.
Raheem Sterling aliongeza la pili la dakika za mwisho na kufanikisha ushindi huo dhidi ya Shakhtar Donetsk na ushindi wa mara ya pili katika ligi ya mabingwa kwenye kundi F kati ya mechi mbili.
Shakhtar wenyewe walikuwa na fursa, kombora la mchezaji wa Brazil Marlos lililokolewa na kipa Ederson huku mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Facundo Ferreyra akipiga hedi ilioponyoka kutoka yadi sita nje.bbc
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment