Kiongozi wa kikundi chenye itikadi kali za imani Charles Manson - ambaye aliongoza mauaji ya kikatili miaka ya 1960 - amefariki dunia katika jimbo la California baada ya kuwa gerezani kwa zaidi ya miongo minne .
Alikuwa na umri wa miaka 83.
Mwezi Agosti 1969 wafuasi wa kundi lake waliwauwa watu saba, akiwemo mcheza filamu wa Hollywood actress Sharon Tate, ambaye alikuwa akitarajia kupata mtoto na mumewe mwongozaji wa filamu Roman Polanski.
Manson alihukumiwa kifo mwaka 1971, lakini kifungo chake kilibadilishwa na kuwa cha maisha jela.
Aliamuini mauaji hayo yangeanzisha vita vya kijamii na hivyo kumuwezesha kuchukua mamlaka.
Manson alilazwa katika hospitali ya Bakersfield iliyoko California mapema mwezi huu na baadae akafa kifo cha kawaida Jumapili.
Mmoja wa wafuasi wa Manson, Susan Atkins, alimdunga kisu Tate hadi kufa na kuuburuza mwili wake uliokuwa ukichuruzika damu hadi mbele ya mlango wa nyumba ya mchezaji filamu huyo.
Wengine wanne waliokuwa nyumbani kwa Tate waliuliwa kinyama kwa kuchomwa visu.
Siku iliyofuatia, matajiri wawili wa Los Angeles- mke na mume , Leno na Rosemary LaBianca, pia waliuliwa na wafuasi wake.
Mauaji hayo yalitambuliwa kwa ujumla kama mauaji ya Tate-LaBianca.
Katika tukio jingine tofauti Donald Shea, mchezaji filamu mwingine wa Hollywood , na Gary Hinman, pia waliuliwa na wajumbe wa familia ya Manson.
Manson hakuwepo kwenye tukio la mauaji, lakini alipatikana na hatia ya kuongoza mauaji ya wafuasi wake katika mauaji yote saba.
Alihukumiwa mwaka 1971.
0 comments:
Post a Comment