Mahakama ya Juu Kenya imetupilia mbali kesi mbili zilizokuwa zimewasilishwa kupinga uchaguzi wa marudio, imeidhinishwa ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.
Rais Kenyatta sasa anatarajiwa kuapishwa Jumanne wiki ijayo.
Jaji Mkuu David Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.
Kesi ya mbunge wa zamani Bw Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif zimetupiliwa mbali.
"Uchaguzi wa 26 Oktoba umedumishwa, sawa na ushindi wa Bw Kenyatta. Kila upande utasimamia gharama yake," amesema.
Uamuzi wa kina utatolewa katika kipindi cha siku 21.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais wa marudio akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.
Kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.
Jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo. Hiyo ni asilimia 38.84.
0 comments:
Post a Comment