Marcus Rashford alikuwa kivutio baada ya Manchester United kufuzu moja kwa moja kucheza michuano ya ligi ndogo ya ulaya (Europa League) baada ya kuwachapa Bournemouth katika mchezo wao wa ligi uliokuwa wa kiporo.
Timu hizo hazikuweza kuukamilisha mchezo huo siku ya jumapili baada ya kuhisiwa kuwepo bomu katika moja ya viti vya mashabiki.
Wayne Rooney alikuwa wa kwanza kuiandikia bado United baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Antony Martial kabla ya Marcus Rashford kupachika la pili na baadaye Ashley Young kumalizia la tatu.
Goli la tatu na la ushindi kwa United liliifanya timu hiyo kukaa juu ya Southampton,ambao wataingia katika michuano midogo ya ligi ya Ulaya (Europa League) lakini kwa kuanzia hatua ya makundi msimu ujao.
Kwa sasa Mashetani hao wekundu wanaamishia makali yao katika mchezo wa fainali ya FA utakaochezwa Jumamosi dhidi ya Crystal Palace kwenye dimba la Wembley.
Louis van Gaal, ambaye bado hatima yake haijajulikana ndani ya timu hiyo anataka kuiongoza United kupata taji lake la kwanza tokea walivyoshinda ligi kuu ya England mwaka 2013 chini ya Sir Alex Ferguson. BBC
0 comments:
Post a Comment