mwanazuoni

TRUMP: NINAWEZA KUZUNGUMZA NA KIM JONG - UN



Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini kuhusu mpango wa nyuklia wa taifa hilo.
“Ninaweza nikazungumza naye, Siwezi kuwa na tatizo kuzungumza naye,” Bw Trump alisema kuhusu Kim Jong-un.
Mkutano huo ungekuwa tofauti kabisa na msimamo wa muda mrefu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini.
Hatua hiyo imemfanya mgombea anayeongoza katika kinyang’anyiro cha chama cha Democratic Hillary Clinton kumshutumu Bw Trump na kusema anashangaza kwa kuwaenzi sana viongozi wababe wan chi za nje.
Taarifa iliyotolewa na mmoja wa wasaidizi wa Bi Clinton imesema sera ya mambo ya nje ya Bw Trump usio wa maana yoyote.BBC
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment