linzi umeimarishwa nchini Hong Kong, huku Zhang Dejiang afisa wa
ngazi ya juu zaidi kutoka Uchina akizuru eneo hilo, tangu maandamano ya
kidemokrasia ya mwaka wa 2014.
Polisi wapatano 6,000 wametumwa
katika eneo hilo na mawe yaliyoko barabarani yameunganishwa kwa nta ili
kuzuia waandamanaji kuyang’oa na kuyatumia kama silaha.
Aidha utawala wa eneo hilo umejenga ua wenye urefu wa mita mbili kuzuia umati wa watu.
Makundi
kadhaa ya wanaharakati wa kijamii yamesema kuwa yanapanga kuandamana
wakati wa ziara hiyo, huku baadhi yao wakipanga kuandamana hadi jengo
kuu la serikali kati kati mwa mji, ambako hafla maalum ya kumlaki Bw
Zhang itafanyika.BBC
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment