HATMA
ya mawaziri watano wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma sasa
iko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, kufuatia hatua ya wabunge wa Chama
cha Mapinduzi kutaka watendaji hao wajiuzulu. Habari za kuaminika
kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika jana mchana
mjini hapa zimesema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua kulifikisha
suala hilo mikononi mwa Rais Kikwete kwa uamuzi zaidi.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kimewataja wabunge wanaotakiwa kujiuzulu kuwa ni pamoja na waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment