Habari ndugu JOSEPH
MIHANGWA?Mimi ni miongoni mwa wadau wakubwa wa makala zako katika
gazeti la RAIA MWEMA zinazoitwa NASAHA ZA MIHANGWA.Katika nakala ya
gazeti hili ya tarehe 03/04/2013 uliandika mada iliyokwenda kwa jina
la MAHAKAMA YA KADHI NA UZANDIKI WA WANASIA UCHARA.Kuna hoja kadha
ambazo ulijaribu kuzizungumzia katika makala hii kama ifutavyo;
i)Mahakama ya kadhi na ofisi ya
kadhi kugharamiwa na serikali
ii)Mahakama zetu zimepewa uwezo wa
kusikiliza kesi na kuamua kwa haki bila ubaguzi
iii)Kuruhusiwa kwa misingi ya
kidinikatika jamiiya kawaida hupelekea mifarakano na mitafaruku
inayoweza kutishia ustawi wa jamii.
iv)Madai ya kidini huwa na ajenda ya
siriukafananisha na chui ndani ya ngozi ya kondoo na ukatoa mafano
yale yaliyotokea Algeria na India.
v)Je taasisi hiyo haitaenda kudai
mfumo mpya wa kidini kuhusu elimu,sayansi, technolojia,mabenki,bima
na uhusiano wa kimataifa ili kukidhi matakwa ya sehemu
moja ya jamii kwa misingi ya dini?
Kimsingi yapo
mengi uliyoyazungumzia kwenye makala yako na kuyatolea ufafanuzi
lakini hayo ni machache mbayo nimeona kuyatolea maelezo ili nijaribu
kukufanulia na pengine utaweza kunielewa na kupata ufahamu mpana juu
ya mahakama ya kadhi.Vilevile uweze kuandika vizuri juu ya hili kwa
mustakabali wa taifa na watu wake.
Kwahiyo kila namba ya hoja hapo juu
itawakilishwa na maelezo ya namba hiyohiyo hapa chini;
i)Kuhusu serikali kugharamia
shughuli za kadhi na ofisi yake-Ni kwamba serikali kugharamia
shughuli za kidini hapa nchini si mara ya kwanza wala si jambo la
kushangaza ila inawezekana likawa la ajabu na la kushangaza kwa
WAISLAMU,Kwasababu ni aghalabu sana kwa serikali kufanya
hivyo.Unakumbuka mwaka 1992 serikali ilipo iingia mkataba na taasisi
za kidini yaani TEC na CCT?Mkataba uliokenda kwa jina la MEMORANDUM
OF UNDERSTANDING (MOU). Katika mkataba huo serikali inawajibika
kugharamia huduma za jamii za WAIKRISTO kama vile shule za seminary
na hopsitali za waikristo.Gharama zinazotolewa na serikali ni za
mishahara kwa wafanya kazi, marekebisho ya taasisi hizo na mambo
mengine yote ambayo yanahitajika gharama ya fedha .
Kwahiyo kuhusu gharama ya
uendeshaji wa ofisi ya kadhi ni wajibu wa serikali na si swala la
ajabu hapa nchini kwetu.
ii)Kuhusu uwezo wa mahakama za
serikali kusikiliza kesi na kuamua kwa haki bila ya ubaguzi-ni kweli
kwamba mahakama zetu zimepewa uwezo wa kusikiliza kesi na kuamua kwa
haki lakini nadhani umeshindwa kuelewa vizuri kuhusu mahakama ya
kadhi , yenyewe inashughulika ndoa,talaka,mirathi na mahusiano baina
ya waislamu wala haingilii watu wasiokua waislamu na haihusiki na
kesi zilizonje ya hizo.
Hivyo basi kwakua serikali
inaruhusu watu wake kufunga ndoa kufuatana na misingi ya dini zao
basi haina budi kuwaachia raia wake uhuru wa kuendesha taratibu za
ndoa zao kufuatana na misingi ya dini yao, kwasababu haiezekani ndoa
ifungwe msikitini chini ya Shekhe alafu matatizo yanayohusu ndoa
yakitokea yakashughulikiwe kwenye Mahakama za serikali ,badala yake
matatizo yote yanayohusiana na ndoa,talaka na mirathi kwa waislamu
yashughulikiwe na Kadhi.
Zipo baadhi ya nchi ambazo
zina mahakama za serikali na zina uwezo wa kuendesha na kusikiliza
kesi na nyengine zina idadi ndogo za waislamu lakini bado zimewapa
waislamu uhuru wa kuwa na mahakama ya kadhi, Kwamfano;
*Kenya katika katiba yao ibara ya
66(3) wanaruhusu mahakama ya kadhi
*Uganada ambayo ina 12% ya waislamu
lakini katika katiba yao ibara ya 129 inaruhusu mahakama ya kadhi
*Gambia katika katiba yao ya pili
(1997) ibara ya 120(b) inaruhusu mahakama ya kadhi
*Nigeria katika katiba yao(Federal
republic of Nigeria 1999) ibara ya 262(2) na 277 inaruhusu kadhi
Sasa hizo ni baadhi ya nchi za
kiafrika ambazo pamoja na ubora wa mahakama zake lakini zimewapa
uhuru waislamu wa kufuta sheria zake katika maswala ya ndoa,talaka,
na mirathi .Itakua Tanzani ambayo mahakama zetu zina mlundikano wa
kesi na maamuzi yasiyosthili yanayowafanya watu wasionacho ndio
wahukumiwe kwa kukosa lakini mafisadi wanaoiba mabilion ya ya fedha
kuishia mtaani kwa kushinda kesi je ni kweli mahakama zetu zina uwezo
wa kuendesha kesi?
iii)Kuhusu mifarakano na mitafaruku
inayotokana na kuanzishwa kwa misingi ya kidini -Ni kwamba matatizo
hayo hayatokani tu kutokana na kuanzishwa na kwa mahakama ya kadhi
bali hutokana na matatizo mengi yanayowakabili wananchi katika jamii
zetu kwamfano halingumu ya maisha,matabaka kati ya walionacho na
wasionacho,ukosefu wa ajira na mengine mengi,ndiyo yanayochochea
wananchi kupamabana na tabaka tawala.
Lakini pia viongozi wa dini husababisha
mifarakano katika jamii na mauaji kwa mfano ;Mauji ya kimbari nchini
Rwanda ,waliokamatwa kwa kiasi kikubwa ni Maaskofu na wachungaji
ambao ndio wachochezi wa kuu wa mauaji hayo.Walikua wakitangaza
makanisani kuwa wanaostahili kuongoza ni WATUSI na si WAHUTU,hali
hiyo ilipelekea wahutu wakikimbilia makanisani kuuwawa na hivyo
hukimbilia Misikitini kama sehemu yao ya amani.
Vilevile umezungumzia kuhusu
vita vya BIAFRA vya mwaka 1967,lakini kumbuka si tu mifarakano ya
kidini ndio yaliyopelekea vita hivyo bali hata kauli za baadhi ya
viongozi wa Afrika zilizokua zikichochea Kujitenga kwa taifa hilo
zilipelekea vita hivyo kwamfano;Mwl. Nyerere alikuwa akichochea
kujitenga kwa taifa hilo.Haya yalisemwa na Jenerali Ulimwengu katika
kipindi cha Malumbano ya hoja.
iv)Kuhusu madai ya kidini kuwa na
ajenda ya siri-Ni kwamba katika madai haya ya mahakama ya kadhi sisi
waislamu wa Tanzania sio wa kwanza kudai bali zipo nchi nyingi ambazo
zilianza kudai na kufanikisha kupata mahitaji hayo kama nilivyo
kuonsha hapo juu.Na katika nchi za jirani yani Kenya na Uganda huu
mfumo wa mahakama wanao na ni zaidi ya miaka 15 na haijawahi kutokea
hata siku moja vurugu zilizosababishwa na uanzishwaji wa mahakama
hiyo na wala ajenda yoyote ya siri ambayo imeziathiri nchi hiyo
kutokana na mahakama ya kadhi. na badala yake ni amani na utulivu
katika uendeshaji wa mahakama hiyo.
Kwa hiyo sisi waislmu wa
Tanzania hatuna ajenda yayate ya siri kwa serikali wala taifa hili
juu ya uanzishwaji wa mahakama ya kadhi ,isipokua tunataka haki yetu
ya msingi katika mirathi ,ndoa na talaka.Mbona Tanzani ni miongoni
mwa nchi mbili barani Afrika ambazo zina ubalozi wa Vatikan ?
Lakini nchi nyingi za kiafrika hazina
ubalozi huo na waislamu wa nchi hii hatujalalamika kuwa uwepo wake ni
ajenda ya siri ya KANISA KATOLIKI?
v)Hatuna haja ya kwenda kudai mfumo
mpya wa kidini kuhusu elimu,sayansi,teknolojia na mengine ambayo
umeyasema kwa sababu;
ELIMU-Tunazo shule zetu za msingi
na za sekondari ambazo zinatoa elimu kulingana na mfumo wa
kiislamu,sio nyingi kama za kwenu lakini hizohizo chache tunazo kwa
mfano;Shule ya sekondari ya kiislamu Ubungo,Shule ya sekondari ya
kiislamu Kirinjiko,Luqmani,Ridhwaa,Kinondnoni,ununio pamoja na
nyengine nyingi.Vile vile tunacho Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro
ambacho kinatoa elimu kwa misingi ya kiislamu,vyote ni vyombo muhimu
katika kutoa elimu kwa vijana wetu kwa mfumo wa kiislamu,pia zipo
taasisi nyingi za elimu ambazo zinashughulika na mfumo wa elimu ya
kiislamu na elimu ya kawaida.
MABENKI NA BIMA-Pia tunazo
taasisi zetu za fedha ambazo zinatoa huduma kwa misingi ya
kiislamu.Kwamfano;
Amana Bank pamoja na benki nyengine za
kawaida ambazo zina mfumo wa kiislamu katika baadhi ya huduma zake
kwa mfano;Stanbik Bank na Natinal microfiance Bank(NMB).
SAYANSI NA TEKNOLOJIA-Pia tuna
taasisi za teknolojia kama Redio za kislamu mfano;Radio
Imani,Kheri,Sauti ya kuran na Tv Imani pamoja na nyengine nyingi
zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika kuwaelimisha waislamu.Zipo pia
Hospitali kama nile Aljumaa Hospital ya Daresalama(Karoakoo)na
Ahmaddiya Hospital ya Morogoro na nyengine zikuzitaja ambazo hutoa
huduma ya afya kwa waislamu na wasiokua waislamu kwa taratibu na
mfumo wa dini yetu
Katika mwezi wa 03 mwaka huu
,Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete alifanya ziara katika Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro ambapo
alifungua jengo la sayansi na ujenzi wa jengo jipya la Teknolojia ya
habari (ICT) ambalo litakapokamilika litashughulikia utoaji wa
teknolojia ya habari kwa waislamu hapa nchini.
Hivyo hatuna sababu ya
kiuanzisha mfumo mpya kuhusu hizo sekta ulizozitaja isipokua
tunachangamoto ya kuziendeleza ili tuweze kukabiliana na changamoto
za waislamu katika nchi hii pamoja na kutopata msaada kutoka
serikaini lakini taratibu ishallah tutafika tunapodhamiria kufika.
Tulichokikosa sisi waislamu wa nchi ni
uhuru wa kushughulikia wenyewe kesi zetu zinazohusu ndoa,talaka na
mirathi kwa misingi ya uislamu.
Hivyo
mi nadhani ungetumia muda wako mwingi katika kuyazungumzia matatizo
ambayo watanzania yanawapata katika nchi hii.Kama vile unongozi
mbaya,rushwa,maradhi,umasikini uliokithiri,ubovu wa miundombinu
yetu,tatizo la ajira,huduma mbovu za afya na kufeli kwa wanafunzi
wetu.Na mengineyo mengi amabyo ungewagusa watanzania moja kwa moja
,na sio kuanza kuponda mahitaji ya dini za wenzio kwani yatakupelekea
kudharaulika na watu na kuonekana kama mchochezi wa vurugu za vurugu
za kidini kwasababu tayari swala la mahakama ya kadhi lishakubaliwa
na serikali kwani ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha
mapinduzi ,na lipo katika hatua ya awali ya utekelezaji.
ALLY AMIRI RWAMBO,
0717743549/0765394591
0 comments:
Post a Comment