Mhe Mbunge Peter Msingwa wa kwanza kulia |
1. ‘Kimsingi nimeonyesha msimamo kwamba nampinga kwa sababu hatendei haki
chama na ndio msimamo wa kamati kuu, tunachoamini ni kwamba tunatakiwa kupigana wote… kwenye matukio yote muhimu yenye maana ambayo ni ya kukijenga chama hatujashirikiana nae, hatujalia pamoja hatujafurahi pamoja, wenzake tulifurahi pamoja Tarime hakuwepo, tumelia pamoja Arusha wenzake wote mara mbili, Iringa, Morogoro hajakuwepo’
2. ‘Bungeni tumedharauliwa tumetukanwa kwenye matukio yote haya ya msingi hajakuwepo lakini kibaya zaidi amekuja na Waraka huu ambao amefanya na mwenzake Kitila, Waraka wa kukigawa chama kwa hiyo mambo kama haya ndio nimeamua kuonyesha msimamo wangu hadharani na naamini Wabunge wengine ambao tuko nao wataendelea kujitokeza siku zinazokuja kwamba hatuko nae kwenye swala hili hata yeye mwenyewe nimeshaongea nae uso kwa uso, sijali nani ni nani… i don’t care’
3. ‘Mimi ni bora nichukiwe katika uhalisia, sitaki kupendwa kinafiki kama mtu ananichukia ni sawa lakini msimamo wangu ndio huo na kwamba Zitto Kabwe hastahili kuwa Naibu Katibu mkuu wa chama chetu’
0 comments:
Post a Comment