mwanazuoni

DR JAKAYA MRISHO KIKWETE AFANYA MAAMUZI MAGUMU

Rais Jakaya Kikwete ametia saini hati ya dharura (Certificate of Urgency) Muswada wa Fedha wa Mwaka 2013 ufanyiwe marekebisho ya kuondoa tozo ya kodi kwa kadi za simu.
Bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 lilipitisha kodi ya Sh1,000 kwa kila kadi ya simu, hatua ambayo ilipingwa na wabunge wengi.
 Aliyasema hayo jana Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia ndugu January Makamba " maana yake ni kuwa muswada huu unatakiwa urudi bunge haraka ili huweze kufanyiwa marekebisho hayo" alisema kabla ya kufikia kwa hatua hiyo raisi alishawahagiza wadau wanahusika na sekta hiyo wakae na kujadili suala hilo la kodi.
Hata hivyo, alisema suala la muswada huo kurudishwa bungeni linategemea na ratiba huku akisisitiza kuwa
licha ya Bunge kupitisha muswada huo tangu Julai, mwaka huu, bado kodi hizo zilikuwa hazijaanza kutozwa.
Julai 23, mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza mamlaka zinazohusika na kodi na mawasiliano pamoja na kampuni za simu za mikononi, kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi hiyo.
Alitoa kauli hiyo alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa kampuni za simu za TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel, Ikulu, Dar es Salaam.
Alisema lengo kuu la kukutana huko lilikuwa ni kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la Sh178 bilioni ambazo zitapotea katika bajeti iwapo kodi hiyo itafutwa.
Wakati wa mvutano wa kodi hiyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alinukuliwa na vyombo vya habari akisema tozo hiyo haikuwa ya kuwaumiza wananchi, bali mapato yake yalilenga kwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini.

Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment