mwanazuoni

CHADEMA KUMECHAFUKA KABLA YA 2015







Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa temeke bw. Yona amepigwa na kuumizwa vibaya Leo usiku na kutupwa maeneo ya ununio. Yona amekuwa ni akipinga vikali maamuzi ya kamati kuu CHADEMA kuwavua uanachama dkt Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na Zitto Kabwe. katika sakata linaloendelea CHADEMA. Huyu ni mwanachama wa 3 kukumbwa na kipigo baada ya katibu wa mbunge dkt Alex kupigwa maeneo ya tegeta, mjumbe wa kamati kuu kupigwa ndani ya kikao na sasa mwenyekiti huyu wa temeke. Kabla ya hapo Samson Mwigamba alipigwa mbele ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe. 
Baada ya kushindwa hoja uongozi wa chadema umeamua kutumia mabavu na kujeruhi watu wanaopingana nao kimawazo

KILICHOMPONZA MWENEYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA TEMEKE NI HIKI HAPA


Taarifa yake inasema ‘Mimi Patrick Y.Joseph ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ninayeshikilia nyadhifa mbalimbali, Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia chaguzi mbali mbali za ndani ya chama, migogoro hii hupelekea mpaka kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika kwa lengo mahalumu.

Chanzo: Picha kwa hisani ya Millad ayo
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment