mwanazuoni

TEGEMEO:TAFAKURI YANGU JUU YA MWENENDO WA CHAMA CHA MAPINDUZI


BARUA YA WAZI KWA WANA CCM WENZANGU…..

Kwa Muda Mrefu Nimekuwa Nikishuhudia Malumbano, Kukosoana na hata Kutukanana kwa Baadhi ya Wanaccm Wenzangu Juu ya Makundi ya Wagombea Uraisi Watarajiwa.Tumeshuhudia Matamko Mbalimbali Yaliotolewa na Viongozi wa Jumuia,UVCCM na Hata Viongozi wa Chama,CCM.

Lakini Nimekuwa Nikiuliza Baadhi ya Maswali Bila Majibu…..
Hivi Matamko Haya Yanamnufaisha Nani??Yanainufaisha CCM Kama Taasisi au Baadhi ya Makundi ndani ya CCM?? Hivi Ule Utaratibu wetu wa Kujadili Mambo ndani ya Vikao,Umeisha au Bado Upo??

Mimi Sijawahi Kuona Wana CCM Tunakosoana kwenye Vyombo vya Habari,Utaratibu wetu ni Kukosoana ndani ya Vikao.Mimi Ninaamini sio Dhambi kwa Mwana CCM yeyote Kutaka Kugombea Uraisi kwa Ticket ya CCM,Ila Kama Amekosea Kufuata Utaratibu Lazima Aitwe kwenye Vikao Halali vya Chama na Aonywe.Tunayo Kamati Kuu,Inayojumuisha Viongozi Makini na Wawajibikaji,Tunalo Balaza la Wazee Lenye Mamlaka Makubwa sana,Baraza la Wazee linaweza kuwaita wale wote wanaotaka Kugombea Uraisi na Waliokwisha Kuanza Kampeni Kinyume na Utaratibu na Kuwaonya.Jamani Mitafaruku Hii miongoni mwa Wana CCM Inatuludisha Nyuma sana,Tunaacha Kupambana na Wapinzania Tunaanza Kupambana Wenyewe kwa wenyewe.Inasikitisha Unapoona Mwana CCM Ameweka Picture ya Edward Lowasa Kwenye Mitandao ya Kijamii na Kuandika Kichwa cha Habari’’Huyu ni Fisadi,Mwizi Hatumtaki na Hawezi Kuwa Amili Jeshi Mkuu ,Mwenyekiti wa CCM na Wala Kuwa Raisi wa Nchi Hii’’Sasa Najiuliza,Kama Kuna Mtu Hatakiwi Kwani Si Atakataliwa Kwenye Vikao Halali ndani ya Chama??Kuna Sababu gani ya Kuanza Kulumbana Kwenye Mitandao ya Kijamii??Bila Shaka Ipo NEC,Chombo Kikuu chenye Mamlaka ya Kuwachuja Wagombea Uraisi kwa Ticket ya CCM,Kama Mtu Hatufai,Naamini NEC Itafanya Kazi Yake.

Mimi Wasiwasi wangu ni Kwamba,Kama Samweli Sitta Akichafuliwa Leo na Sisi Wana CCM Wenyewe kwenye Mitandao ya Kijamii na Vyombo vya Habari,Kesho Kama Akifanikiwa Kupitishwa na NEC,Itatuwia Vigumu Kumsafisha Maana Wapinzani Watakuwa Wameshapata Sehemu ya Kutushambulia.
Lakini Pia Nimekuwa Nikijiuliza,Hivi Baraza la Wazee la CCM Limesahau Majukumu Yake?Maana Baadhi ya Wajumbe wa Balaza la Wazee Kama Mzee Malecela nay eye Pia Anatoa Matamko kwenye Vyombo vya Habari,je Ameshindwa Kutumia Balaza Kuwaita Wote Walioanza Kampeni na Kuwaonya??
Ukweli ni Kwamba Hakuna TAMKO Litatolewa Kwenye Vyombo vya Habari Likawa na Manufaa kwa CCM Kama Taasisi Bali Litakuwa na Manufaa kwa Baadhi ya Makundi ya Ugombea Uraisi ndani ya CCM.

UJUMBE MFUPI KWA UVCCM
Vijana Wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi,Hebu Tuache Kutumika na Wagombea Uraisi Watarajiwa,kwa sasa Tupambane Kuimalisha CCM, Kwa Maana CCM Ikiwa Imara,Hata Kama Tukisimamisha Jiwe Litapita.Mimi Najua Kabisa,Viongozi wengi ndani ya UVCCM Wamefanikwa Kupata Nyadhifa Hizo kwa Sababu Wapo Baadhi ya Wagombea Urais Watarajiwa Waliwapa MSAADA wa KIFEDHA kwa Ajili ya Kampeni Wakati wa Mchakato wao wa Kutaka Kuiongoza UVCCM.

Kwa Maana Hiyo,Hata Nyie Mnaotoa Matamko Kwenye Vyombo vya Habari Hamna UZALENDO WOWOTE,Mlisha Nunuliwa……
Jamani Chama Kwanza Mtu Baadae…Maana Sote Tupo ndani ya CCM na Kama CCM Ikifa Leo Hautapata Platform ya Kutoa Matamko Unayoyatoa Leo Hii.Tutasambaratika Kama Kupe Waliomwagiwa Dawa ya Kuuwa Wadudu.CCM ni Yetu Wote,Hakuna Mtu ndani ya CCM Mwenye Hati Miliki ya CCM,Bali Sote kwa Pamoja ndio Tunaunda na Kuimalisha CCM.
ANGALIZO (CAUTION)
Najua Wapo Wanaccm Wanaokitumia Chama Cha Mapinduzi kwa Maslahi yao Binafsi na sio kwa Maslahi ya Wanaccm wote na Maslahi ya Watanzania kwa Ujumla.Watu Hawa Wanafahamika,Lazima Tuwaogope Kama UKOMA na Lazima Wachukuliwe hatua za Kinidhamu kama Italazimika Kufanya Hivyo kwa Manufaa ya CCM.
MATAMKO Kwenye Vyombo vya Habari Yanayolenga Kuwakosoa Wanaccm ni SUMU kwa CCM Yenyewe,Tuwe Makini na Matamko haya……Maana Yanatudhoofisha,Tuludi kwenye Asili yetu ya Kujadili Mambo ndani ya Vikao.

USHAURI kwa Kamat Kuu ya CCM

Hakuna Mtu Aliebora ndani ya CCM kuliko CCM,Ni Mbaya Sana Kama Kuna Mtu ndani ya CCM Anakuwa Maarufu na Nguvu Kuliko CCM.Ni vema Tujifunze toka kwa Majirani zetu Chadema,leo hii Wanamwaga DAMU Juu ya Zitto Kabwe Maana Zitto alikuwa Maarufu Kuliko Chadema.Nasema ni Bora Tumwage Jasho Kipindi Hiki Katika Kuwaonya na Kuwakemea Hawa WAROHO wa URAISI,Wanaoanza Kupiga Kampeni wakati Comrade Jakaya Mrisho Akiwa Madarakani,WAROHO wa Uraisi Wanafahamika,Haina Haja ya Kuorodhesha Majina yao kwa Ujumla.Tafadhari Naomba Wachukuliwe Hatua Maana Wanaendelea KUKIVURUGA Chama cha Mapinduzi na Kujenga Makundi ndani ya Chama.
Ikiwa Mtaendelea Kuwaacha Hawa WAROHO wa MADARAKA Waendelee Kujijenga,Kujiimalisha na Kupata Umaarufu Mkubwa Zaidi ya CCM Basi Tujiandae Kuona Wagombea BINAFSI Wakitoka ndani ya CCM.
Naamini na Ninauhakika Kabisa ya kwamba WAROHO hawa wa Madaraka Wanaoendelea Kujinadi,Kununuwa Vijana ndani ya CCM na Kuwapigia Kampeni ndani na nje ya CCM Hawatakubali Kuachia Nafasi ya Uraisi Pale Watakaposhauriwa na Kamati Kuu, Ku Step Down na Kuwaachia Wana CCM wengine wapepelushe Bendera ya CCM Katika Kinyang’anyiro cha Uraisi.Waroho Hawa Wanatumia Pesa Nyingi sana hivyo Nasema Tena Hawatashaurika Itakapofika Wakati wa Kura za Maoni,Hivyo Watakuwa Tayari WANG’ATUKE Ndani ya CCM na Kugombea Uraisi kwa Ticketi ya Vyama Vingine vya UPINZANI
Hivyo ni Bora Kamati Kuu ua CCM Ipambane na waroho Hawa wa Madaraka Mapema Kabla ya Wao Kuitikisa na Kuivuruga CCM. Kamati Kuu Iwaonye WAROHO Wote wa Madaraka Wanaoonekana na Wasioonekana kwa Macho.
Kama Kamati Kuu ya CCM Itaendelea Kuwaacha,Kuwafumbia Macho WAROHO Hawa wa Madaraka Waendelea Kupiga Kampeni,Ifahamike ya kwamba Waroho hawa Wataendelea Kuteka Akili za Wana CCM na Watanzania kwa Ujumla Hivyo Chama Kitapata Shida sana Pale Kitakapopendekeza Mgombea Mwingine wa Uraisi nje ya Mategememo ya Watanzania na Wana CCM Walio wengi.
Ifahamike ya Kwamba Siasa ni Maisha,Siasa ni Uhai na Ikiwa Tutaendelea Kuwafumbia Macho WAPUUZI Wachache Waendelee Kuivuruga na Kujenga Makundi ndani ya CCM Basi Watanzania Watapoteza Matumaini na Imani yao Juu ya CCM Kama Chama Imara na Thabiti.
Nitakuwa Muaminifu na Kuitumikia CCM kwa Nguvu Zote na Sio Kumtumikia Mtu Fulani ndani ya CCM.
CCM Kwanza Mtu Baadae…..
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment