HOTUBA YA ZITTO KABWE YA JANA PALE MWEMBE YANGA
Dar es Salaam ina historia ya kipekee ndio sehemu ambayo juhudi zote na harakati zote za kuikomboa nchi yetu ziliendeshwa hapa. Wazee wa Dar es salaam kwa kipindi kile walikuwa vijana akina Abdlwahd Sykes, Dosa Azizi na wengineo wengi waliendesha harakati za kuikomboa nchi yetu katika mkoa huu na ikasambaa kwenda mikoa mbalimbali licha ya kwamba kuna mikoa ambayo ilichangia kwa nguvu zaidi kama mkoa wa Tanga. Lakini bado juhudi zote ambazo lifanya harakati za kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye makucha ya wakoloni zilifanyika hapa mkoani kwetu Dar es Salaam. Sisi ACT WAZALENDO baada ya kuzunguka mikoa yote kama mlivyotajiwa tumeamua leo 04 Julai 2015 kuja Dar es Salaam kukileta chama chetu kwenu na kuja kuwakabidhi chama hichi ili kwa pamoja tuungane kuweza kujanga siasa mpya katika nchi yetu, mnafahamu leo sio mara yangu ya kwanza kuja kuzungumza hapa Mwembe Yanga. mara ya kwanga nilizungumza hapa Mwembe Yanga tarehe 15 sept 2007. hapa pana historia ya kipekee kwa sababu hapa ndio sehemu ambapo kwa pamoja vyama vyote vya upinzani viliungana nasi wakati wa harakati za mkataba wa Buzwagi na tukaja mbele yenu tukawatajia watu ambao walikuwa wanarudisha nyuma harakati za nchi yetu kama mnakumbuka tulitaja hapa harakati za orodha ya mafisadi 11 ndani ya mwembe yanga. Tuliona kwamba ni vizuri historia hiyo isipote Mwembe Yanga leo tena tuje Mwembe Yanga na tuzungumze na watu wa Mwembe Yanga lakini hili ambalo litakuwa linaenda na lile la 2007 tutaliweka mwisho kwenye hotuba yetu ili tupate muda wa kutosha wakuelewa na muweze kutuelewa na hatmae muamue kutuunga mkono , sisi kama chama tumeamua kuja na Azimio la Tabora kama ilivyoelezwa na viongozi wezangu, watu wengi wanajiuliza kwa nini Azimio la Tabora? wengine wasema kwa nini atukuliita tu azimio la Arusha, wananchi wa Dar es Salaam . Tabora mwaka 1958 ndipo wazee wetu walikutana kufanya uamuzi ambao uliarakisha uhuru wa nchi yetu, uliaharakisha uhuru wa kisiasa wa nchi yetuwale ambao wanasoma historia wanakumbuka kitu kinachoitwa Uamuzi wa Busara wa Tabaora 1958.
Ni uamuzi ambao ulikiacha chama cha TANU kwenye matatizo kwa sababu ndipo ambapo chama kile kiligawanyika na mzee Zuberi Mtemvu akaanzisha chama kingine cha ANC na hakina mwalimu wakabakia na chama cha TANU lakini maamuzi yale yalipelekea nchi yetu ipate uhuru mapema zaidi tofauti na ambavyo ilikuwa imetarajiwa mwaka 1967 wazee wetu walikutana Arusha wakati ule walikuwa ni vijana mwalimu alikuwa ni kijana, Kambona alikuwa ni kijana wote walikuwa ni vijana , walikutana Arusha sababu ya kukutana Arusha hali ambayo ilianza kutokea katika nchi yetu. ambapo viongozi ambao walipewa mamlaka baada ya uhuru walianza kutumia mamlaka yale kujinufahisha wao wenyewe. ndio maana wazee wakaamua kuja na aAzimio la Arusha ili kuweza kuondoa hiyo mbegu ambayo ilikuwa imeanza kupandwa mbegu ya watu kujipandikizia mali, wakati ule walikuwa wanaitwa waBenzi kwa maana kwamba walikuwa wanaendesha mabenzi kama ilivyokuwa wakoloni hivyo ikawa wakoloni weusi umemtoa mzungu umemwingiza mweusi lakini mweusi yule akawa anafanya yale yale ambayo mzungu alikuwa anafanya. Uamuzi wa Arusha Azimio la Arusha ilikuwa lifanyikie Tabora 1968 kwa sababu mwalimu alitaka miaka 10 ya uamuzi wa busara ufanyikie Tabora lakini baadae kutokana na ilikuwatika nchi waliamua kukutana Arusha na kutoa azimio la Arusha lilikuwa na mambo manne tu kimsingi. la kwanza walikuwa wanaelezea chama cha TANU wakati ule, la pili lilikuwa linaeleza siasa ya ujamaa na la tatu lilikuwa linaelezea siasa ya kujitengemea na katika eneo hili la tatu ndipo tuliamua kutaifisha mabanki yote, kutaifisha viwanda vyote , kutaifisha taaasisi za bima na kuendesha uchumi wa dola yaani decentralized economy na ya nne ilikuwa miiko ya uongozi na wezangu wakaniomba nizungumzie hili la nne la miiko ya uongozi, miiko ya uongozi wakati ule ilianzishwa hili kupambana na viongozi wa kisiasa ambao walikuwa wanatumia nafasi zao za kisiasa ili kujilimbikizia mali ndio maana mwalimu alikuwa mkali sana. leo hii ukisoma ile miiko unaweza kushangaa ukasema wazee wetu walikuwa wanawaza nini wakati mwingine ? kwa mfano ilikuwa ni marufuku kwa kiongozi wa umma kuwa na nyumba ya kupangisha jambo ili uwezi kulisema leo kila mtu atakukatalia, ilikuwa ni marufuku kiongozi kuwa na hisa katika kampuni ya kibepari au kikabaila sasa hivi leo kila mwanasiasa anafanya biashara anaendesha makampuni wakati ule ilikatazwa ili kuweza kuondoa mgongano wa kimaslai na ili ndio eneo ambalo sisi tunaliona ni tatizo kubwa katika nchi yetu, wananchi wa Dar es salaam leo hii ufisadi imekuwa ni kasha katika nchi yetu ufisadi umekuwa tu si kasha tu bali ni wimbo na kila mtu anasema kwamba yeye akiwa na nafasi ya uongozi au wao chama chao kikishika madaraka wanaweza kuondoa ufisadi lakini hakuna mtu ata mmoja mwanasiasa awe wa chama tawala au vyama vya upinzani ambaye anaeleza unaondoa je ufisadi " the how" unaondoa je ufisadi kwa sababu watu wanadhani kuwa watu wakati wa mwalimu Nyerere apakuwa na rushwa , rushwa ilikuwepo ndio maana palikuwa na sheria ya rushwa lakini wakati wa mwalim Nyerere apakuwa na ufisadi kwa sababu kulikuwa na miiko ya uongozi , viongozi walikuwa wanabanwa na miiko kujilimbikizia mali toka mwaka 1992 mara baada ya nchi yetu kuondokana na azimio la Arusha ka kuleta azimio la Zanzibar hali ya nchi imekuwa mbaya sana baada ya kufanya vile wakauza viwanda vyote waliujiuzia nani wao wenyewe. leo hii uoni ajabu waziri wa kilimo kuwa na kampuni ambayo ina zabuni ya kusambaza mbolea ataacha kujipendelea? leo hii sio ajabu waziri wa mali asili na utalii kuwa na vitalu au hoteli kwenye mbuga za utalii atacha kujipendelea? leo hii si ajabu kuwa na waziri wa nishati na madini ambaye kampuni yake ina tenda ya kuuza umeme Tanesco ataacha kujipendelea ? hapo ndipo tuanona umuhimu wa kuwepo kwa miiko ya uongozi kwamba lazima ifikie wakati mwanasiasa anapoamua kufanya siasa na anapoamua kuwa kiongozi wa umma basi aweke pembeni shughuli zake za kibiashara. kwa sababu tusipofanya hivvyo lazima kutakuwa na mgongano wa maslai, leo hii bunge letu limejaa wafanya biashara sio vibaya ni haki yao ya kikatiba hakuna ubaya hata hata kidogo lakini ni namna gani tunafanya ili kuzibiti mtu kutumia nafasi yake ya ubunge au ya uwaziri au uwaziri mkuu au ya umakamu wa uraisi au urais kujipendelea yeye au yeye na familia yake au yeye na ndugu zake. Wananchi wa Dar hakuna namna yoyote ya kupambana na ufisadi katika nchi yetu kama atutarudisha miiko ya uongozi .mtu yoyote atakaye kupa suluhisho tofauti na hilo anatafuta nafasi yake ya kula ataki kuleta mabadiliko kwa hali ya nchi yetu ilivyokuwa ni lazima tuwe na radical changes ni lazima tufanya ambayo ayafikiliwi ni lazima tufanye mapinduzi katika nchi yetu hali ilivyo sasa hivi uchumi wa nchi yetu unashikwa na watu wachahche wachache mno na ndio maana sisi tuna historia ya kuwa nchi ambayo ina uchumi ambao unakuwa kwa kasi lakini umasikini auondoki kwa sababu uchumi huo unashikwa na watu wachache, hatuna namna yoyote tunayoweza kufanya zaidi ya kufanya uchumi umilikiwe na watu wengi zaidi hakuna namna yoyote ya kufanya wananchi wa Dar zaidi ya kuonyesha ya kwamba tunataka tufanye uchumi wetu uwe inclusive na watu wafanye kazi watu wafanye shughuli watu tusiwatumie tu katika shughuli za kisiasa lakini tuwafanye azima vijana wafanye shughuli mbalimbali za kiuchumi. Haya ndio tunayaeleza katika azimio letu la Tabora . tumesema kwamba mtu yeyote ambaye anayetaka kuwa kiongozi wa chama chetu kiongozi wa kushika ofisi ya umma ni lazima anapogombea aingie mkataba na chama cha kwanza atakachofanya ni kuweka mali zake madeni yake na masilahi yake hadharani ili wananchi waweze kuona hili atakapokuwa anashiliki kwenye maamuzi yenye maslahi yake wananchi waseme hapana una maslahi hapa uwezi kufanya maamuzi hapa. hii ndio mfumo wa maadili ya uongozi ambao tunataka kutengeneza katika nchi yetu. Wananchi tumeshawapa kila aina ya uoza ambao upo serikalini , tumeshawapa kila aina ya mfumo mbovu unaopelekea ubazilifu katika nchi yetu . kila mwaka hivi sasa mkisikia mkaguzi wa hesabu kuu za serikali anatoa taarifa yake wengine msahasema ahaa tumeshazoea kila siku yanatoka hakuna lolote linalochukuliwa , siku hizi hata mtu akiamka akasema jamaniee kuna sehemu kuna ufisadi kuna wizi wananchi mnasema haaa kauna mtakalofanya hii ndio hali tunataka kuibadilisha katika nchi yetu.
Na ndio maana watu wanajiuliza kuna watu wenzetu wanasema kwamba nyinyi Zitto na wenzako mnakwenda kuanzisha chama si amuoni kuwa si mtagawa kura. sisi tunawaambia ndugu zetu na naomba mnisikilize watu wa Temeke mnisikilize vizuri na watanzania mnaotusikiliza mwaka 2000 watanzania waliopiga kura walikuwa watu milioni 8 walipiga kura na walikwenda kwenye masaduku yao kupiga kura. mwaka 2005 wakati Kikwete anachanguliwa kwa mara ya kwanza watanzania milioni 11 walikwenda kupiga kura, milioni 3zaidi waliongezeka . Mwaka 2010 watanzania waliopiga kura walipiga kura ni milioni 8 walirudi chini asilimia 42% tu ya watanzania waliopiga kura . Chuo kikuu walifanya utafiti ni kwa nini watu awapigi kura? jibu kubwa walilopata takribani ya asilimia 60% ya hojaji ikawa watanzania wamekata tamaa wameona katika watu wote waliongombea na vyama vyote vilivyogombea hakuna ambaye anaweza kuleta mabadiliko ndio maana awakwenda kupiga kura. wananchi wa Temeke Sisis tunakwenda kuwatafuta hawa asilimia 58% ambao awapigi kura waje kutupigia kura sisi na hizi asilimia 42% tuwaachia wengine wagawane wenyewe , na tuna kila sababu wananchi wa Dar es Salaam. moja sisi uongozi wetu umeundwa na watu ambao wana rekodi ambazo hata watu wajaribu namna gani kuzifuta aziwezi awizekani kwa sababu zimeandikwa na zipo juhudi nyingi zinatumika kuzifuta juhudi hizo lakini awawezi kwa sababu zimeshaandikwa na zipo. wananchi wa Dar kabla ya mwaka 2005 nchi hii ilikuwa inaendeshwa katika sekta ya madini hovyo hovyo ilifikia wakati waziri aliweza kuondoka Dar es Salaam na brificase yake akaweka na mikataba na kwenda uingereza hotelini na kasaini na apakuwa na watu wanaweza kusema.
Lakini aliyezungumza nanyi mbele yenu kiongozi wa ACT Wazalendo alisimama kidete na kuzungumza. na Leo hii tunapozungumza sheria ya madini ni mpya na sera ya madini ni mpya na sio hivyo kwa muda zaidi ya miaka kumi makampuni ya madini yalikuwa ayalipi kodi leo kufatia kazi ile kazi ambayo tulifanya 2007 leo yanalipa kodi ya mapato kama makampuni mengine kwa sababu ya kazi 2007. nimesikitika juzi jana na leo kuhusu miswada mitatu ya gesi ambayo serikali ya chama cha mapinduzi kimeipeleka bungeni kwa hati ya dharura ili iweze kupitishwa, wananchi wa Dar es Salaam maswala ya ya mafuta na gesi ni maswala mabayo atutakiwi kufanyiwa haraka ni mswala ambayo yanahitaji ushirikishwaji mkubwa wa wenye mali ambao ni nyinyi watanzania. N i maswala ambayo yanahitaji concentration kubwa ya wadau wote sio maswala ambayo mnaweza kuyalazimisha mkayapeleka bungeni kwa sababu mpo wengi mkayapitisha halafu tukawaingiaza watanzania katika matatizo makubwa . Sisi tumeyasema haya katika zidhara zetu zote na tunayarudia hapa kwamba kitendo cha wabunge wa kambi ya upinzani kupinga miswada isijadiliwe ni kitendo cha ushujaa kinachopaswa kuungwa mkono na kila mtanzania.
Juzi nilikuwa na wezangu mkoa wa Lindi na Mtwara kule ndipo ambako gesi watanzania tunajivunia gesi ipo wananchi awajui chochote kinachoendelea , wabunge wao awajazungumza nao kwenda kuwashaurisha kuhusu miswada inayokwenda bungeni. Zanzabar kila siku wanalalamika wanalalamika kwamba sisi upande wa bara tunawaonea tunawaminya ,wanasema koti la muungano linawabana . Moja ya jambo ambalo la zanzibar wanalalamikia ni mafuta na gesi kwamba leo hii ni jambo la muungano lakini dhahabu na alimasi si jambo la muungano. unawaeleza nini wazanzibari? vikao vimekaa wakubwa wamekubaliana kwamba mafuta na gesi mafuta na gesi vinaondoka katika orodha ya mambo ya muungano. Rasimu ya Katiba ya mzee Wariba imeyaondoa katika mambo ya muungano na rasimu ya katiba iliyochakachuliwa ya Chenge imeyaondoa katika mambo ya muungano. Leo serikali ya chama cha mapinduzi inapeleka miswada bungeni ya mafuta na gesi ambayo inatambua mafuta na gesi ni mambo ya muungano. kama sio kuwacheza sherei na kuwatukana wazanzibar ni nini? wakilalamika wanzibari leo tutanasema nini? tuna haraka gani?na haya ndio mambo ambayo wananchi tunayazungumza yakwamba hapana na pale tunapozungumzia mambo yanyohusu mambo yanayohusu rasilimali za nchi yetu ni lazima watanzania wote tuseme hapa tufanye kazi bila ya itikadi za kisiasa natumewaambia watu wa lindi wawaambie wabunge wao bila ya kujali vyama vyao na tumewaambia watu wa Mtwara waambie wabunge bila ya kujali vyama vyao kwamba miswada hii isubuli lije bunge la kumi 11 kwa sababu hili bunge hata wabunge awakai bungeni viti vipo wapi wanaingia kusaini posho tu wanarudi wanakwenda majimboni kwao watajadili namna gani miswada hii.
wananchi sisi tumeanzisha chama hiki pamoja na kwamba tuna itikadi ambayo tukiiamini siku zote pamoja na kwamba tuna mawazo ambayo tunayaamini siku zote , tumeanzisha chama hiki kama sehemu ya mchakato wa kuhimarisha demokrasia , na watanzania kazi ambayo mnatakiwa kuifanya ni kusikiliza na kuwa pima watu na kuamua mchele ni upi na pumba ni zipi? Wenzetu kila sehemu tuliokuwa tunaenda kufanya mikutano wenzetu awataki awataki tufanye mikutano wanafanya kila aina ya hila tusisikilizwe, sasa demokrasia gani ? ambayo hairusu watu kusikilizwa. Nyinyi ndugu zangu wananchi wa Temeke mnajua nimepewa kila aina ya majina , nimepingwa kila aina ya mishale , chama hiki ndio jukwaa ambalo pamoja na mambo mengine lazima nieleze jamani kuwa hali ilikuwa hivi na tumeamua kufanya hivi, wenzetu hawataki kusikia hayo. Nataka kuwaambia watu wa Temeke sisi tumezamilia tumezamilia kujenga chama tofauti tumezamilia kujenga chama ambacho kitarudisha Tanzania kwenye misingi.
Na tunawaomba watu wa Dar es Salaam muungane mkono na sisi msisikie propaganda za maasimu wetu, maasimu wetu wanazunguka mikoani wanasema Zitto na chama chao ni wasaliti wametusaliti. sasa kuna baadhi ya maneno tulikuwa tunawambia wananchi , wananchi hivi ni mara kwanza vyama vya siasa kurushia maneno, hivi nyie wananchi mmesahau ya kwamba miaka miwili iliyopita kuwa wabunge wa chama kimoja waliwaita wabunge wenzao mashoga wakapigana mesahau mmesahau? leo si wapo pamoja wanashirikiana ? kwenye siasa ni lazima uongeze na za kwako. Hivi wananchi wa Temeke atukuaminishwa kwamba mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI Mbatia mara baada ya kuteuliwa na Kikweteamabye ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi ,amkusikia Mbatia anaitwa mbunge wa viti maalum wanawake amkusikia Mbatia anaitwa pandikizi amkusikia anaitwa shushsushu leo hii wapo pamoja na Mbatia wanafanya siasa ndio siasa kwenye siasa ongeza na zako. Ndio maana tunawataka wananchi lazima lazima mtuangalie wanasiasa na mtupime kulingana na matendo yetu mtupime kulingana na historia , juzi nilikuwa Tanga kwamba kama kuna mbunge ambaye ameangusha serikali ya Chama cha Mapinduzi mara nyingi zaidi hakuna anayenizidi.
Miaka mitatu mfurulizo 2012,2013 na 2014 tumeangusha serikali kwa kuwaondoa mawaziri wa Chama Cha Mapinduzi na hakuna ambaye anaweza kulinganishwa na kazi ambayo tumeifanya. Hakuna msaliti hakuna mtu ambaye nafanya kazi na Chama Cha Mapinduzi anaweza kupeleka hoja ya kutaka kumg'oa waziri mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. haukana hakuna na anayeweza kufanya hivyo ni mtu ambaye anataka kujenga misingi ya uwajibikaji katika nchi na ndio kazi tunayotaka kuifanya na ndio kazi tunayotaka kuifanya ndani ya ACT Wazalendo, ndio maana tunawaomba watu wa Dar es Salaam mtupokee na ndio maana tunawaomba watu wa Dar es Salaam mkipokee chama hichi mkiangalie na mkipokee na muamue kukilea. Kwa sababu ni chama ambacho kinalenga jukwaa la watu ambao wanataka kufanya siasa za kweli na sisi hatuna kinyongo na mtu yeyoteanayetaka kufanya siasa ya ukweli, siasa usafi siasa ya maadili anayaetaka kurejesha miiko ya viongozi tufanye naye kazi tuokoe wananchi tuokoe watoto wa Tanzania. Tuakikishe wananchi wa Tanznaia wanakwenda vizuri.
Ndugu wananchi mwaka 2012 mwezi Novemba niliwakilisha hoja Bungeni nikiwa mbunge kipindi kile kabla ya hapo kulikuwa kuna ripoti imetoka ya vyombo vya habri mbalimbali duniani , ambayo inaelezea namna gani ambavyo nchi za kiafrika zinapoteza mapato mengi sana kwa sababu au watu binafsi au makampuni kukwepa kodi na kuficha pesa ughaibuni, baada ya kufanya utafiti ni kaamua kupeleka hoja binafsi bungeni hoja ile lengo lake lilikuwa ni kuitaka serikali kufanya uchuguzi wa kina ili kuweza kutambua ni kiwazo gani cha fedha ambacho watu wa Tanzania au makampuni ya Tanzania yameficha katika mabanki mbalimbali ya nje. Serikali tukaipa miezi sita bungeni , miezi sita ikapita ikaomba tena miezi sita miezi sita tena mengine ikapita. Leo tunapozungumza ni miaka miwili na miezi sita serikali bado ijafanya ile kazi na kuiwasilisha bungeni kama jinsi ambavyo tulivyoiagaiza. Tumejitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kwa kadri ya uwezo wetu kuiambia serikali kwamba ile kazi ambayo mliagizwa na bunge ya kuchuguzi watu ambao wanatorosha pesa na kuzificha nje tafadhali kazi ile iwasilishwe Bungeni ili hatua ziweze kuchukuliwa na serikali ikaweka nta kwenye masikio mpaka sasa ichafanya hivyo.kwa maana hiyo wananchi wakabaki na sintofahamu ya kwamba shughuli hii inakwenda je? na kwa bahati mbaya sana wabunge wezangu ambao waliobakia bungeni nao pia wameacha jambo hilo bila kuhoji jambo kubwa sana. Na nitawapa takwimu wananchi , la kwanza kuna sehemu nyingi sana ambazo watu wanaotorosha fedha wanaweza kuficha fedha zao . Sehemu inayozungumzwa sana ni Uswiz lakini kuna visiwa ambavyo vipo chini ya imaya ya waingereza na Jersey. ambavyo na venyewe watu vina watu wengi wanaficha pesa.
Huko Jersey ndipo Chenge alikutwa ameficha zile dola Million Moja. kwa mujibu wa takwimu wa serikali ya Jersey zinaonyesha kwamba watanzania ambao fedha ambazo zipo katika mabenki yao ambao watejea yaan client ni watanzania zina thamani ya Paund za uingereza Million 440 amabazo ukizitafisiri kwa fedha za kitanzania takribani shilingi sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.06
Huku Uswizi kuna mabenki mengi sana lakini benki kuu ya Uswazi ina utaratibu kila mwaka kutangaza depost yaani akiba ambazo watu ambao sio raia wa uswiz wameweka katika mabenki ya Uswizi.Na kuna watu wameweka fedha halali na kuna watu wameweka fedha haramu kuna watu ambao walikuwa wafanyakazi ni watanzania wanaishi nje ni lazima wafungue akaunti nje kwa ajili ya kuendesha shughuli zao na kuna watu ambao ni wafanya biashara ambao shughuli zao za kibiashara ni lazima wawe na akaunti nje kwa ajili ya kufanya transactionwanafanya lakini kuna utaratibu wa kisheria.
Utaratibu wa hapa nchi kwetu ili uweze kuwa na akaunti nje ni lazima upewe kibari na gavana wa benki kuu.
Tulitaka serikali ifanye uchuguziili tuweze kufahamu hizi za Jersey karibia trlioni 1.05 na hizi za Swizi kama dola za kimarekani dola 305, je fedha zipi zinawateja halali na kwa shughuli halali ? Serikali mpaka leo imechimba na aijatoa majibu. Baada ya kutoa hoja ile bungeni na kupitishwa na bunge , mataifa mashirika mengi yalikuwa yananihita katika mikutano yao kwa sababu Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza ambayo iliweza bunge kutoa azimio ikiliagaiza serikali kuchuguza mambo haya. Hivyo walikuwa wanataka kujua muendelezo ukoje muondelezo ukoje. Mwaka 2013 nilikwenda Ufaransa nikakutana na jaji, Jaji ambaye alikuwa anafanya uchuguzi kuhusu wafaransa ambao wamefichA fedha Uswizi katika mafile ambayo aliyapata akapata na mafile yaliyokuwa yanayowahusu watanzania kwahiyo akaniita kasema hii vipi? tukachukua nyaraka zile tukapeleka serikalini , tukachukua nyaraka mpaka siku hizi za karibuni tukampa gavana wa benki kuu , tukampa kamishina generali wa TRA, tukampa mwanasheria mkuu tukawaambia hawa ambao awana uchungu na sisi wanatupa nyaraka hizi kwa nini nyinyi amtoitaarifa mpaka leo ndugu zangu watanzania , sasa katika mazingira kama haya hakuna namna yeyote ambayo mtu unaweza kufanya zaidi ya kufanya shindikizo la mwisho na bahati mbaya ni kwamba watu wana akaunti katika mabenki mengi sisi tumepata taarifa katika benki mmoja katika tawi lake moja. Benki ya HSBC ya Swizland ambayo katika taarifa ina watu 99 niwatanzania, sisi tunachokifanya tunajua kwamba ndani ya taarifa kama hizi kuna watu gemen kabisa wanafanya kazi zao wanafanya shughuli zao kwa vyovyote vile unaweza kuwarudika katika kundi la watu wanaotorosha fedha wakati wanafanya shughuli zao. Tumegawa orodha hii kwa waandishi wa habri wote ambao wapo hapa, umewapatia ? wapatie. Kila chombo cha habari kipate. na wananchi wa Tanzania hakuna namna yoyote ambayo tunaweza kufanya ili kuishindikiza serikali ya chama cha mapinduzi kutekeleza maazimio ya bunge zaidi ya kuhakikisha kwamba watanzania wanapata haki ya kujua.hakuna na namna yoyote kwa sababu tumevumilia miaka miwili na ziada ili serikali itoe taarifa bungeni lakini serikali imegoma kutoa taarifa bungeni. kwa miaka miwili wananchi wa TEMEKE tumevumilia hakuna namna ya kufanya zaidi ya kuhakikisha wananchi wanapata taarifa hizi na waandishi wa habari wanapata taarifa hizi. ili kuishindikiza na taarifa hizi ndugu zangu ni taarifa za banki moja tu na ni za tawi moja la banki hiyo ni zaidi ya dola miillion 114 za kimarekani tu na nchi moja tu. serikali ina mengi kwa sababu imefanya uchuguzi kwa muda mrefu tunataka kuishindikiza serikali kuhakikisha ya kwamba taarifa hiyo yenye mengi zaidi alzima itolewee hatuna namna yoyote ya kufanya.
Wananchi wa Dar es Salaam na wananchi wa Temeke kama alivyozungumza katibu mkuu na kama alivyozungumza Mwenyekiti wetu wa kitaifa wa chama tumekuja kukileta chama hiki kushindana kwenye uwanja wa kisiasa na lengo letu kuleta aina mpya ya siasa na ndio maana tumekuja na azimio la tabora kuonyesha tofauti yetu na vyama vyingine vya kisiasa lengo letu wananchi wa Temeke wananchi wa Mwembe YANGA ndio maana kwenye mkutano wetu uoni tunamtukana kwahiyo tunawataka wananchi wa Temeke tunawataka wananchi wa Dar es Salaam. Kama tulivyofanya kwenye mikoa mengine tumekuja ili mtupe nguvu ili tuweze kufanya makubwa zaidi.
watu wanasema wasomeee..... Kuna mambo ya kisheria kuna mambo ya kisheria ambayo ni muhimu sana ambayo yanaweza kushughulikiwa kwa sababu ya serikali ya chama cha mapinduzi imeshindwa kuwajibika katika bunge kimetufikisha hapa.
Na amini kuwa waandishi wa habari mtaweza kuwahoji kila watu walikuwa kwenye orodha hii na kuweza kuwatarifu umma. kuna watu humu wanausika katika tuhuma za rada na kuna watu wanamiliki makampuni. " kuna mambo ya kisheria naomba mnielewe"
kuna watu hapa wanausika katika kashifa ya rada na walikuwa wanahusishwa kuficha fedha katika mabenki ya uswizi. majiana nayo ona hapa kwa watu wa rada kwa mfano Mnamjua mtua anaye miliki SHIVACOM mnamjua Somaia, waandishiwa wa habari mtaliona jina hilo namba 38. ambaye ni mmiliki wa shivaCom.
Najaribu kuangalia ni namna gani naweza kuendaana na mambo ya kisheria.
MWISHO
Imeandaliwa na Mshana Junior
0 comments:
Post a Comment