Watanzania tuache ujanja ujanja,hatuwezi kujiita wasomi kama hauwezi kutenda yale tunayoyajua.
Kama hatuwezi kutenda yale tunayoyahubiri,
Nyanja zote tatu za kujifunza lazima zishirikiane ili wasomi wetu walete tija.
Wengi wanakosoa wakipewa fursa wanafanya yaleyale,na hapa nitafafanua kidogo.
Kwa mujibu wa Mwana saikolojia Benjamin Bloom.
Ameonyesha kuwa ili kuwa na jamii iliyoelimika ni lazima nyanja zote zikamilike.
1.Cognitive domain-hii ni nyanja ya akili kuwa na uwezo wa kufikiri kwa kiwango kinachotegemewa.
Affective domain-hii ni nyanja ya kuwa na hisia na hamu ya kufanya Jambo.(emotion)
3.Psychromotor domain-hii ni nyanja ya kutenda yale tuliyojifunza.
Sasa watanzania wengi tunajua saaana kusema na kuweka
mikakati,tupo vizuri sana kuandika project mbalimbali,tunaweza sana
kukosoa jambo linalofanya na mtu mwingine.
Hii ni kiashiria cha kukua Kiakili,yaani utambuzi ni Mkubwa sana.
Pia wananchi wengi huwa tunakuwa na hamu/hisia ya kufanya mabadiliko.
Watu wanajitoa hata kwa kuandamana kuonyesha kuwa wameguswa na jambo flani wanalolijua kutikana na kupevuka kifikra.
Unapozungumzia Psychromoter (Utendaji)hapo ndio wengi tunaposhindwa.
Tunaweza sana kusema,kuhamasisha na hata kushawishi lkn
huyo msemaji anapopewa fursa aongoze jambo flani analolijua
vizuri,hushindwa kutenda yale aliyokuwa akiyahubiri.
Hii ipo nyanja nyingi sana za maisha hapa Tanzania.
1.Soka.
Watanzania wengi ukiwakuta wanachambua soka,unaweza kujua kuwa wapo vizuri lkn unapofika muda wa kuwakabidhi timu waiendeshe ,timu inashuka daraja.
Watanzania wengi ukiwakuta wanachambua soka,unaweza kujua kuwa wapo vizuri lkn unapofika muda wa kuwakabidhi timu waiendeshe ,timu inashuka daraja.
2.Siasa
Watanzania wengi tunaweza sana kupanga mikakati ya
kisiasa na kuonyesha udhaifu wa wanasiasa wengine,lkn tunapopewa
kuongoza siasa tunafanya yaleyale.
Mfano Mzuri ni Makala nzuri za Prof Muhongo juu ya Nishati na Madini enzi akiwa hajateuliwa kuwa waziri.
Alikosoa madudu mengi ya serikali kupitia gazeti la Raia
Mwema lkn alipokabidhiwa wizara ili atende yale aliyokuwa
akiyasema,ameishia kwenye tuhuma ya wizi wa fedha kwenye account ya
Tegeta Escrow.
Chadema wamekuwa wakisoaji sana wa ccm juu ya ukosefu wa
demokrasia ndani ya chama cha mapinduzi,walipoaminiwa kidogo tu na
watanzania,Wakafanya zaidi hata ya ccm,Maana ukomo wa Madaraka kwenye
katiba uliondoshwa ili kuendeleza ufalme kwenye chama.
Wakati wa mchakato wa katiba mpya,tulishuhudia viongozi
wasomi na tunaowaamini wakishabikia upuuzi,wakakubali sifa ya mbunge iwe
kujua kusoma na kuandika ,wakafuta maoni ya wananchi na kuweka yale ya
kulinda maslahi yao.
Baada ya tibaijuka kufukuzwa kazi,akaanza kujifanya prof,na
sasa anatoa mawazo yakukosoa katiba ambayo wakati anadhamana alishindwa
kuitendea haki.
Hata watia nia ambao sasa ni Mawaziri ndani ya serikali ya
sasa,wooote kiliochao ni ufisadi na rushwa ambayo kwa mamlaka waliyo
nayo wangeweza kupambana nayo lkn hakuna utendaji (Psychromotor)
Watanzania wenzangu,tutende yale tunayoyasema,tutende yale tunayoyakosoa,tuishi katika maneno yetu.
Hakuna namna lazima Cognitive,Affective na Psychromotor viende kwa pamoja.
Tukifanya hivyo Mabadiliko ya kweli yanayoweza kuifanya Tanzania iwe kama Maleysia na Singapore yanawezekana.
J.K.Maarufu
0765733718/0714276818
0 comments:
Post a Comment