Hakuna huyo unaemwita Muarabu Zanzibar.
Wala hakuna Muarabu anaetaka kuja kuitawala Zanzibar.
Hao wanaoitwa Waarabu ni Akina Mansour Yusuf Himidi mtoto wa Fatma Jinja
na baba yake ni Mwafrika Brigadia Yusuf Himidi babu yake ni Salim Jinja na
yeye pia kachanganya damu vizazi na vizazi.
Hao wanaoitwa Waarabu ni akina Shadya Yusuf Himidi.
Hawa wote ni Wazanzibari kama Abeid Amani Karume alivyokuwa Mzanzibari.
Wala sina haja ya kukueleza asili ya Karume na lini wazee wake waalifika Zanzibar
kwani haina maana yoyote.
Amani Abeid Karume kachanganya damu na kapata kuwa Rais wa Zanzibar na
mkewe Bi Shadya kawa ''First Lady,'' na ''Uarabu,'' wake.
Mababu na mababu wamezaliwa na kuzikwa Zanzibar sasa zaidi ya miaka 200.
Hilo la Waafrika kuuzwa utumwani limefanyika na hakuna atakaepinga lakini
limefanyika pia katika Transatlantic Slave Trade si Zanzibar peke yake.
Historia hii ni maarufu inajulikana.
Nasikitika kuwa sasa unaanza kunilisha maneno.
Wapi nimesema mimi sijali maisha ya Waafrika?
Nani kakwambia jela ya mateso ni ya ''Muomani mmoja.''
Abdallah Kassim Hanga ni Mzaramo katolewa jela ya mateso kwenda kuuawa.
Hanga hakuwa na tone hata la mbali la Kiarabu.
Mimi nikimjua vyema kabisa.
Si yeye tu baba yangu alikuwa na marafiki zake wawili Jaha Ubwa na Abdulaziz
Twala wakitembeleana.
Wameuliwa.
Aman Thani ni Mshirazi si Muomani asili yake Iran ndiyo alipopata jina la
Aman Thani Fairuz.
Fairuz ni jina la ki-Persia.
Unataka kufanya mjadala wa Zanzibar ilhali historia ya Zanzibar wewe mgeni nayo.
Hili halitawezekana.
Unachekesha.
Bahati mbaya unaniandikia Kiingereza sijui kwa nini na mimi huchukia sana kumjibu
Mswahili mwenzangu kwa Kiingereza.
Yuko mtu hapa nilimuonya kuhusu tabia hiyo nikamwambia mimi nina Merit Pass First
Class English Oral, Cambridge 1970 na nimekuwa katika mradi wa Oxford University
Press East Africa wa kusomesha Kiingereza na nimeandika vitabu viwili katika mradi
huo vinasomeshwa Kenya na Uganda (isipokuwa Tanzania) na nikaweka na picha za
vitabu vyangu.
Hakuna wa kunitisha kwa Kiingereza.
Nikamuonya aache kunichomekea Kiingereza.
Hajarudi tena hapa Majlis.
Unachekesha.
Waarabu kama unavyopenda kuwaita wameuliwa katika mapinduzi kwa kuwa
babu zao walikamata watumwa.
Hii ndiyo hoja yako?
Soma ''Nuremberg Trials.''
Wajerumani wengi Manazi walinyongwa baada ya Vita Vya Pili kwa falsafa kama
hizi unazoleta leo.
Namaliza kama ulivyomaliza wewe.
Hiyo ''reverse gear'' kuelekea ''Arab domination,'' itatokea wapi?
Au kwako wewe Maalim Seif na Ismail Jussa ni Muarabu na Muhindi?
Ugozi.
Hebu pitia orodha ya wagombea uchaguzi Zanzibar kisha nipe orodha ya Waarabu
ambao wewe umewaona mle.
Ati unaniandikia mimi: ''pure and simple.''
Unachekesha sana.
Huu mjadala nauweka katika blog yangu mohammedsaid.com ili dunia ijue
jamaa kutoka Bara wanavyoiona Zanzibar na Wazanzibari na jinsi wasivyojua historia
yake.
Chanzo: http://www.mohammedsaid.com/
0 comments:
Post a Comment