mwanazuoni

Mke wa Trump amnadi mumewe hadharani

Mke wa mgombea urais Marekani kupitia chama cha Republican Melania Trump, ametoa hotuba ya kampeni isiyo ya kawaida kuhusu uchaguzi utakaofanyika Jumanne ijayo novemba 8.
Akizungumza katika jimbo la Pennsylvania, mke wa Trump alielezea majukumu yake kama mama na historia yake ya uhamiaji.
Amesema kuwa mume wake anaipenda Marekani na ameahidi kuifanya kuwa nchi yenye nguvu kwa mara nyingine.
Melania amesema tuhuma anazopewa mumewe juu ya unyanyasaji kwa wanawake ni uongo
Image captionMelania amesema tuhuma anazopewa mumewe juu ya unyanyasaji kwa wanawake ni uongo
Kwa upande mwengine Rais Obama amekuwa akiwashawishi wapigakura vijana katika jimbo la Florida kukiunga mkono chama cha Democtaic na Hillary Clinton.
Donald Trump aliwahi kuhutubia jimboni hapo, kabla ya kwenda North Carolina.
Bi Clinton pia ataenda kufanya kampeni jimboni hapo.bbc
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment