mwanazuoni

REA KUTOA UMEME KWA VIJIJI 348

VIJIJI 348 vya Mkoa wa Dodoma vitapata umeme katika Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu; Imefahamika.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Medard Kalemani alibainisha hayo katika uzinduzi wa Awamu ya Tatu ya REA mkoani Dodoma uliofanyika katika Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi.

“Leo mkandarasi atakabidhiwa vijiji 182 baadaye mkandarasi mwingine ataletwa kwa ajili ya vijiji 166 vilivyobaki,” alisema.

Alisema mkandarasi atakayekabidhiwa vijiji 182 wa Kampuni ya OK Electrical & Electronics Services Limited anatakiwa kufanya kazi usiku na mchana na awe amemaliza kazi katika muda wa miezi 15 katika vijiji alivyopangiwa kazi.

Alisema katika Wilaya ya Bahi vijiji 52 ambavyo havijafikiwa na umeme, vitapata nishati hiyo ukianzia katika Kijiji cha Kigwe.

Dk Kalemani alisema bei ya kuingiza umeme majumbani ni Sh 27,000 na kuwataka wananchi kutumia umeme katika shughuli zao za kiuchumi, kuendeshea mitambo ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na kuanzisha viwanda vidogo na vya kati.

Mbunge wa Bahi, Omar Baduel alisema usambazaji wa umeme vijijini katika wilaya hiyo utaharakisha shughuli za maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Kitundu aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo ili kuunganisha umeme kwenye nyumba zao na kuutumia katika shughuli za kiuchumi.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment