mwanazuoni

Abdi Banda amepata ‘deal’ Afrika Kusini

Na Zainabu Rajabu
BAADA ya Abdi Banda kusimamishwa kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kosa la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar George Kavilla wakati akiwa hana Mpira. Leo Banda anatarajia kukwea pipa kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba na moja ya timu huko Afrika kusini.
Habari za kuaminika ambazo shaffihdauda co.tz imezipata ni kwamba, tayari Banda yupo Dar tangu juzi akifanya utaratibu wa safari yake.
“Ndio naenda Afrika Kusini kwenye mazungumzo na timu moja huko na sitakaa muda mrefu maana naenda kwa mazungumzo kuhusu mkataba na si kufanya majaribio sidhani kama hata wiki itaiha,” alisema Abdi Banda.
Mkataba wa Banda na Simba unaisha mwisho wa msimu huu Banda yuko huru kuzungumza na timu yoyote lakini Simba walimpa mkataba mpya Banda ili ausome na akikubaliana nao ausaini lakini wakala wa Banda alisitisha kusaini mkataba mpya mpaka mwisho wa msimu.
Wakati Banda akiondoka leo kwenda Afrika Kusini kamati ya nidhamu ya TFF itakaa leo pia kupitia shauri lake la kusimamishwa na kamati ya mashindano na usimamizi (kamati ya masaa 72) kucheza mechi za ligi kuu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar.
Wakati Banda akiondoka amesema ana baraka zote kutoka kwa uongozi wa timu ya Simba alisema.
”Nimewaaga viongozi wangu na wanafahamu juu ya hii safari, haya ni maisha yangu kupitia soka hivyo natakiwa niangalie kotekote, nimekosa mechi dhidi ya Mbao nitakosa pia mechi dhidi Toto baada ya hapo nitakuwa nimerudi ila itategemea na maamuzi ya kamati.”
Lakini shaffihdauda.co.tz inajua Banda yuko kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba wa moja ya timu za Afrika Kusini ingawa taarifa za awali zinasema anaenda Kaizer Chief kwa majaribio ya mwezi mmoja.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment