Mtoto mmoja mvulana mwenye umri wa miaka minane katika jimbo la Ohio, aliendesha gari akiwa na dadake mdogo hadi duka la McDolad's baada ya kujifunza kuendesha gari kupitia mtandao wa YouTube.
Jarida na Morning Journal la Ohio lilisema kuwa polisi walipigiwa simu kutoka kwa wenyeji kuhusu mtoto ambaye alikuwa akindesha gari mjini.
Wafanyakazi katika mkahawa wa McDolad's walidhani kuwa ulikuwa ni mchezo wa kuigiza wakati mtoto huyo alisimamisha gari kwenye dirisha kununua chakula.
Mtoto huyo alifuata shera zote za barabara, mtu mmoja aliyeshuhudia alisema.
"Hakugonga chochote njiani, polisi Jacob Koeher kutoka kijiji cha East Palestine alisema.
- Roboti 'mtoto' wa Toyota
- Melbourne: Gari lililoendeshwa eneo la wapitanjia lawauwa 3
- Polisi Afrika Kusini wampata mtoto wa mwezi mmoja aliyetoweka
- Baba afunga kitovu cha mtoto wake na kamba ya kiatu
Mtoto huyo aliwaambia polisi kuwa alijifuza kuendesha gari kwa kutazama video kwenye mtandao wa YouTube.
Inaripotiwa kuwa wazazi wa watoto walikuwa nyumbani wamelala wakati watoto hao waliamua kuchukua funguo za gari.
Baadaye wazazi wao waliitwa kuwachukua na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa.
0 comments:
Post a Comment