mwanazuoni

Athletico Madrid wawapa somo Mbao Fc na wengineo

Hakuna kazi kubwa kama kujenga timu, huwa inahitaji muda sana kuikuza timu hadi iwe na mashabiki wengi na ni jambo ambalo linahitaji moyo wa uvumilivu sana laa sivyo unaweza kukata tamaa mapema.
Nchini Hispania Athletico Madrid kwa sasa wanakua kwa kasi ambayo vigogo wa La Liga wenyewe wamekuwa wakihenyeshwa, hadithi ya Athletico inanikumbusha vilabu vidogo vya ligi yetu ya Tanzania Vpl.
Miaka michache iliyopita Athletico Madrid walikuwa na wanachama/mashabiki wanaotambulika 30,000 tu(ilikiwa klabu ya kawaida) ukiacha wale mashabiki wengine wa pembeni ambao hawatambuliki.
Lakini kwa sasa baada ya mafanikio makubwa ya miaka ya karibuni yanayotokana na kushiriki fainali za Champions League inasemekana idadi ya wanachama wanaotambulika wa Athletico Madrid imefikia 110,000.
Hesabu zilizofanyika toka mwezi July mwaka jana hadi hii leo klabu hii imepata jumla ya mashabiki wapya 60,000 wanaofahamika ndani ya miezi 10 na hii ni kati ya sababu ya kuhamia Wanda Metropolitono uwanja wao mpya.
Wanda Metropolitono una ukubwa zaidi kuliko Vicente Calderon uwanja wa zamani wa Athletico na hii inamaanisha mapatao ya Athletico Madrid yanakwenda kuongeezeka kutoka kupata mashabiki 56,000 hadi 67,000.
Athletico Madrid iwe somo katika vilabu vyetu, hakuna shortcut ya mafanikio na ukifanya vizuri lazima klabu ikue, hakuna shortcut ni uvumilivu na subira kwani ukubwa wa Athletico na mafanikio yake ya sasa vilijengwa tangu miaka zaidi ya 20 iliyopita.
Hadithi ya Athletico inanikumbusha hadithi ya Mbeya City jinsi walipanda katika ligi na kufanikiwa kuvuta idadi kubwa ya mashabiki kutokana na hamasa na uwezo wa kikosi hicho cha Mbeya.
Hakuna linaloshindikana, timu zikiacha ujanja janja, wakapiga soka na kuacha kasumba ya Uyanga na Usimba na kuamini kuwa zinaweza ni wazi kwamba miaka kadhaa ijayo tutakuwa na ligi yenye vigogo wengi.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment