mwanazuoni

Mahakama ya juu nchini Kenya inaendelea kutoa sababu za kufutwa matokeo ya Urais

Naibu jaji mkuu nchi Kenya Philomena Mwilu, amesema kuwa kushindwa kwa IEBC kufuata agizo la mahakama kuhusu madai yaliyoibuliwa na upinzani, inaonyesha kuwa madai ya udukuzi yalikuwa ni ya ukweli.
Jaji Mwilu amesema mahakama ilikubaliana madai ya upinzani kuwa matokeo yalitangazwa kabla ya matokeo yote kutoka kwa vituo 40,000 kupokelewa.
"Uchaguzi haukuwa na uwazi na hatukuwa na lingine ila kuufuta," jaji alisema.




Jaji Mwilu amesema tume ya IEBC ilitegemea ripoti za waangalizi wa uchaguzi kuamua kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki.
Waangalizi walikosolewa vikali wakati uchaguzi ulifutwa kwa kuharakisha kusema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wenye uwazi.
Kwa upande wake jaji mkuu nchini Kenya David Maraga, amesema kuwa upinzani hakubaini madai yao kuwa kampeni za rais zilitumia fedha za umma kugharamia kampeni zao.



Jaji Maraga amesema kuwa sampuli kadha za fomu zilionyesha kuwa hazikuwa na mihuri rasmi, zingine hazikwa na sahihi na namba za usajili wala alama rasmi
Amesema kuwa uchaguzi haukufutwa tu kwa sababu ulikuwa na hitilafu, lakini kile amekuwa akikichunguza ni ikiwa hitalafu hizo zilishawishi matokeo.bbc
.
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment