Wameelezea kuwa katika kipindi kigumu huku wakitarajia wiki moja inayokuja kuwa wakati mwingine mgumu kwao.
"Msingi wa familia yetu umetuondoka,’’ alisema msemaji wa familia ya Mandela Luteni Generani Themba Matanzima ingawa alisisitiza kuwa Mandela daima atasalia katika mioyo yao.
Watu wameendelea kukesha nchini Afrika Kusini huku wakimkumbuka Mandela.
Msafara wa magari utakaobeba mwili wake Mandela utapita katika barabara za Pretoria kwa siku tatu mfululizo kabla ya siku atakapozikwa Mandela Jumapili tarehe 15.
Maafisa watatangaza wakati msafara huo utakapoanza.
Mandela alifariki Alhamisi usiku akiwa na umri wa miaka 95 nyumbani kwake Kaskazini mwa Johannesburg
Mamia ya waombolezaji walikusanyika nje ya nyumba ya Mandela na kuwasha mishumaa usiku kucha wakiimba nyimbo za kusherehekea maisha ya Mandela.
Luteni Generali Matanzima alimfananisha Mandela na mti wa Mbuyu ambao uliwapa kivuli jamaa na familia yake.
0 comments:
Post a Comment