Leo ni siku ya kihistoria ndani ya nchi ya Afrika ya kusini baada ya kuwa katika majonzi takriban wiki nzima sasa . leo ndio siku ambayo wana Afrika ya Kusini pamoja na wageni wa mataifa mbalimbali wamefanikisha kuulaza mwili wa mpendwa wao.
Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa. Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela wa Thembu.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa wakati safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha, raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na urithi wake.
Mungu ilaze roho ya marehemu peponi amini
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment