mwanazuoni

BIFU LA AZAM NA SIMBA LAINGIA PATAMU


Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC Zacharia Hans Poppe ametishia kuacha kutumia bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya Azam, hii ni kutokana na kuondokewa na kijna wao Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyejiunga na kikosi cha Azam FC ‘Wanalambalamba’ kwa mkataba wa miaka miwili.
Poppe amesema, pesa wanazopata Azam kutoka kwenye bidhaa zao ndizo zinazotumika kufanya ‘udhalimu’ na kumlipa mshahara moja ya kiongozi wao Saad Kawemba ili atekeleze mambo hayo.
“Mimi nahasira na Azam nataka kuanzia sasa hata maji ya Azam sitaki kunywa, bidhaa zao zote sijui keki, ice cream sitaki, kwasababu hiyo hela wanayopata pale ndio wanakuja kutumia kwenye udhalimu huu na yeye Kawemba wanamlipa mshahara aje afanye mambo kama haya”, amesema Poppe.
“Sasa labda tupunguze kipato chao twende katika mambo kama haya?”, alihoji.
Azam wamekuwa wakishutumiwa kuwa, walikuwa wakichochea kuvunjwa kwa mkataba kati ya Simba SC na  Ramadhani Singano ili wao (Azam FC) wamsajili mchezaji huyo kama mchezaji huru.
Bofya hapa chini kusikiliza kauli ya Hans Poppe na story nyingine wakati Rais Kikwete akieleza masuala ya kimichezo wakati analihutubia bunge mjini Dodoma.
Bofya hapo chini usikie mwenyewe…








Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment