Ted Cruz kumzua
Trump leo?
Leo ni siku ambayo huenda tukaanza kumjua mgombea atakayepeperusha bendera nyekundu ya
chama cha Republican dhidi ya bluu ya Democratic hapo mwezi
Novemba katika uchaguzi mkuu wa Marekani. Leo wanachama wa Republic katika jimbo la Indiana wanatarajia kupiga
kula kuchagua wawakilishi 57 wanao waniwa na wagombea watatu yaani Donald Trump seneta wa New York, Ted
Cruz seneta wa Texas na John Kasch gavana wa Ohio. Ili kujihakikishia
tiketi ya kugombea kupitia chama cha
Republican mgombea anatakiwa kupata wajumbe 1237 mpaka sasa Donald Trump
anaongoza kwakupata wajumbe wengi 996
akifuatia Ted Cruz 565 huku
John Kasch akishika mkia 157.
Ifahamike kuwa Indiana ndio jimbo lenye
wajumbe wengi mbali na Calfonia lenye wajumbe 172. Hivi karibuni Cruz na
Kasch walikubaliana kuunganisha nguvu
kwenye jimbo hilo la Indiana ili
kumzuia Trump asipate wajumbe 1237 wanaohitajika
kupata tiketi ya kugombea. Wawili hao hawana nafasi yakupata wajumbe 1237 hata wakishinda kwenye majimbo yalio salia badala yake
wanamatumaini ya kupata tiketi ikiwa mshindi wa mojakwamoja kupitia wapiga kura
atakosekana. Hivyo kurefusha mchakato mpaka kwenye kongamano la Cleveland linalofayika hapo mwezi Julai. kongamano hililo humchagua mtu atakaeonekana
anafaa kwenye chama cha Republican. Hata
hivyo huenda jina la Trump lika katwa
kama mchakato wa kumpata mgombea utaamuliwa na kongamano la Cleveland kwani
Trump haungwi mkono sana na wajumbe wengi wa Grand Old Party (GOP ). Hivyo kuufanya uchaguzi
katika jimbo la Indiana kuwa muhimu sana kwa Donald Trump kukwepa ko ngamano la
Cleveland na pia kwa Ted Cruz na John Kasch wanaotegemea Kongamano la Cleveland ili kupata tiketi ya kupeperusha bendera nyekundu ya wahafidhina wa chama cha Republican.
Mwandishi
Morgan
0 comments:
Post a Comment