Duru za habari kutoka mji ulioharibiwa wa Mosul nchini Iraq, zinasema kuwa raia kadhaa wameuwawa, pale walipokuwa wakiukimbia mji huo, kunusuru maisha yao, dhidi ya mapigano mabaya yanayotekelezwa na wanamgambo wa Islamic State.
Wanahabari wa runinga ya Reuters, wamepata maiti ya wanaume, wanawake na watoto, zikiwa zimetapakaa katika barabara za mji huo.
Hilo limetukia katika Wilaya ya Zanjili, karibu na eneo la mapigano, ambapo jeshi la taifa ya Iraq, linakabiliana vikali na wanamgambo hao wa Dayesh, kama wanavyofahamika.
Mfanyikazi mmoja wa shirika la utoaji misaada la Marekani- Dave Eubank, amesema kuwa wapiganaji wa I-S, wamekuwa wakiwamiminia risasi wananchi wanaojaribu kuutoroka mji huo.
Anasema kuwa ameona maiti 50, lakini kwa msaada wa jeshi la Marekani linalosaidiana na wanajeshi wa Iraq, amefaulu kuwaokoa watu wawili tu.BBC
0 comments:
Post a Comment