Idara ya polisi Jijini London, inasema kuwa maafisa wake wamewauwa washukiwa watatu wa kisa cha ugaidi kilichotokea kwenye daraja moja Jijini London.
Magaidi hao waliwauwa watu 7 huku wengine 48 wakijeruhiwa.
Idara ya polisi inasema kuwa, washambuliaji watatu kati yao wamepigwa risasi na polisi na kuuwawa.
Ghasia zilianza baada ya gari moja kuingia ndani ya umati wa watembeaji miguu, katika daraja kuu jijini London.
Aliyeshuhudia ameiambia BBC kuwa, aliwaona watu watatu wakiwa na visu, wakikimbia kutoka katika daraja hilo, kuelekea eneo moja kuliko na soko la Borough.
Anasema kuwa watu hao watatu walianza kuwadunga visu watu kiholela barabarani.
Muda mfupi baadaye, polisi waliokuwa na silaha wakajibu shambulio hilo, huku milio ya risasi ikisikika.
Watu 20 wanasemekana kupelekwa katika hospitali sita tofauti Jijini London.
Mabasi yanaelekezwa kwingine. Daraja la Southwark lililoko karibu pia limefungwa.
Shirika la Uchukuzi London (TfL) limesema babarara ya Borough High pia imefungwa, na taarifa zinasema maafisa wa polisi wenye silaha wameonekana maeneo hayo.
Mwandishi wa BBC Holly Jones aliyekuwepo katika daraja hilo wakati wa kutoka kwa tukio hilo, anasema gari lililohusika lilikuwa linaendeshwa na mwanamume na lilikuwa linaenda kwa kasi ya karibu maili 50 kwa saa.
"Alilipinda gari karibu nami na akagonga watu watano au sita hivi. Aliwagonga wawili mbele yangu na kisha wengine watatu waliokuwa nyuma yangu," Bi Jones ameambia BBC.
Watu hao watano au sita wanatibiwa, amesema.
Bi Jones anasema gari hilo lilikuwa linasafiri kutoka katikati mwa London na lilielekea upande wa kusini wa mto.
Anasema baadaye aliona mwanamume akikamatwa na kutiwa pindi na maafisa wa polisi.
Bi Jones anasema mwanamke Mfaransa ni miongoni mwa waliojeruhiwa.
Tukio hilo ambalo linatukia majuma kadhaa tu baada ya watu 22 kuuliwa pale mhanga mmoja wa kujitolea kufa, alipojilipua ndani ya uwanja mmoja wa burudani huko mjini Manchester, limelaaniwa na viongozi mbalimbali duniani.
Maafisa wa Magari ya kuwabeba wagonjwa wa London, moja ya idara za kwanza kuzungumzia tukio hilo, walisema wanashughulikia kisakikubwa eneo la Daraja la London na kuwatahadharisha watu wasielekee eneo hilo.bbc
0 comments:
Post a Comment