mwanazuoni

MAJINA YA MAWAZIRI WANAOTAKIWA KUJIUZURU

HATMA ya mawaziri watano wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma sasa iko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, kufuatia hatua ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi kutaka watendaji hao wajiuzulu. Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika jana mchana mjini hapa zimesema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua kulifikisha suala hilo mikononi mwa Rais Kikwete kwa uamuzi zaidi.


Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kimewataja wabunge wanaotakiwa kujiuzulu kuwa ni pamoja na waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

CHANZO: TANZANIA DAIMA
Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment