Waziri Mkuu wa Israil, Benjamin Netanyahu, amekwenda Liberia, kushiriki katika mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Afrika Magharibi, ECOWAS.
Israil inazidisha maingiliano yake na nchi za Afrika, na hii ni safari ya pili ya Bwana Netanyahu Afrika, katika mwaka mmoja.
Mfalme wa Morocco, Mohammed wa 6, amevunja mpango wake wa kuhudhuria mkutano huo, kwa sababu ya Bwana Netanyahu kuwepo.
Viongozi hao wa Afrika Magharibi, wanatarajiwa kujadili maombi ya Morocco kutaka kujiunga na ECOWAS, na pia kuchagua mwenyekiti mpya, kuchukua nafasi hiyo kutoka rais wa Liberia, Rais Ellen Johnson Sirleaf.
0 comments:
Post a Comment