Mtawaliwa siku zote anatakakumuigiza mtawala katika maumbile yake, mavazi yake, kazi zake na yoteyanayokhusiana na hali yake na dasturi zake. —Ibn Khaldun
Mapinduzi Tanganyika na Kenya 
Picha kubwa ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 haiwezi kufahamika bila ya kuyafahamuijapokuwa kwa mukhtasari mfupi mapinduzi ya kabla yake yaliofanyika Tanganyika, na baadaye Kenya.Mapinduzi ya Tanganyika, ya Zanzibar, na ya Mwambao wa Kenya ni mifano ya mapinduzi yakalamu na ya umwagaji damu.
Tanganyika iliupata uhuru wake tarehe 9 Disemba 1961na Waislam wa Tanganyikawalikuwa na mchango mkubwa sanakatika kuupiganiya uhuru huo. Hayati Julius Kambarage Nyerere alitowa mchangomkubwa na yeye mwenyewe alikiri hivyo kwenye hotuba yake ya kuwaaga wazeealiyoitowa Dar es Salaam katika mwezi wa Novemba mwaka 1985. Kwa mara ya kwanzaMwalimu alielezeya namna alivyopokelewa, kujuulishwa na kusaidiwa sana na wazee wa Kiislamu wa Dar es Salaam. Kwenye shughuli za TANU yeyealikuwa ni Mkristo peke yake na mara nyingine alikuwepo John Rupia.
Muhimu pia na kwa mara ya kwanzaMwalimu alisikika akisema kwenye hotuba hiyo kuwa hata jina la TanganyikaAfrican National Union (TANU) lilifikiriwa na kuundwa na akina marehemuAbdulwahid Sykes walipokuwa askari Burma katika vita vya pili vya dunia.1
Historia iliyofichwa ya mchangowa Waislam katika kuupiganiya uhuru wa Tanganyika imeandikwa na kuelezwa kwaufasaha mkubwa na mwandishi maarufu wa Tanzania Bwana Mohamed Said kwenyekitabu chake kwa lugha ya Kiingereza, The Life and Times of AbdulwahidSykes (1924–1968), na kwa Kiswahili Maisha na Nyakati za AbdulwahidSykes (1924–1968) Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi yaUkoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Kitabu hicho ni muhimu sana kwa wanaotaka kufahamu vipi Waislam waliupiganiyauhuru wa Tanganyika na namnawalivyopinduliwa kwa mapinduzi baridi kwanza kabla ya kupinduliwa kwa Dola ya Zanzibar tarehe 12Januari 1964. Kilele cha mapinduzi ya Tanganyika ni kudhoofishwa nguvu zaumma wa Kiislamu pale ilipovunjwa East African Welfare Muslim Society (EAMWS)na zilipozimwa juhudi za kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiislam mwaka 1964.2
Bwana Mohamed Said piaamefafanuwa katika kitabu chake Uamuzi wa busara wa Tabora namna ganiuongozi wa Waislam kutokeya African Association mpaka kuundwa kwa TANUwalivyopinduliwa kwa mapinduzi ya kalamu. Baraza la Wazee la TANU ambaloMwenyekiti wake alikuwa marehemu Mzee Suleiman Takadiri lilipinduliwa chali kwakazi iliofanywa na kiongozi na viongozi wa Kiislam waliouweka mbele uzalendo waKiafrika kuliko mafundisho ya dini yao.Chanzo cha mapinduzi hayo yalikuwa masharti matatu yalioikabili TANU katikakushiriki uchaguzi wa kwanza wa Tanganyikawa kulichaguwa Baraza la Kutunga Sheria. Mkutano wa TANU wa Tabora wa tarehe21–26 Januari 1958 uliamua kuingiya uchaguzi wa kibaguzi wa kura tatu ambaoulikuwa na masharti matatu magumu:
1) Ili Mwafrika aweze kupiga kuraalitakiwa awe na kipato cha pauni mia nne za Kiingereza kwa mwaka.
2) Awe na kiwango cha elimu yadarasa la kumi na mbili.
3) Na awe ameajiriwa katika kazimaalumu.3
Uamuzi wa busara wa Taborahaukuwanasa Waingereza kama ulivyowanasa Waislam wa Tanganyika ambao wengi waohawakuweza kuwachaguwa viongozi wao kwa sababu uchaguzi wa kura tatu “ulikuwaukizuia uongozi wa kuchaguliwa kuingia kwenye madaraka.”4
Kwa upande mwengine, Kenya kabla ya kupata uhuru wake tarehe 12Disemba 1963, siku mbili baada ya uhuru wa Zanzibar,ilikuwa imegawanyika sehemu mbili: Koloni la Kenya,au bara, na Himaya ya Kenya,au Mwambao. Sheikh Abdillahi Nassir ni mmoja kati ya viongozi wa Mwambao ambayealihudhuriya mkutano wa Mwambao uliofanyika Lancaster House, London, baina ya tarehe 8–12 Machi mwaka1962.
Anaelezeya Sheikh Abdillahikwenye kanda iitwayo “Mwambao: Historia ya Pwani ya Afrika Mashariki,” kuwaHimaya ya Kenya ilikuwa ninchi kabla ya Koloni la Kenyakuwa ni nchi kwa miaka isiyopunguwa 1,300, na namna chuki za uzalendo waKiafrika zilivyowaathiri Waislam na khasa chuki za kikabila na propaganda yautumwa na Uarabu.5
Sehemu hizo mbili za Kenya, Koloni la Kenyana Himaya ya Kenya auMwambao, zikawa ni nchi moja ya Kenyakwa makubaliyano ya mabadilishano ya barua baina ya Waziri Mkuu wa Kenya, Mzee Jomo Kenyata na Waziri Mkuu waZanzibar Bwana Mohammed Shamte walizoandikiyana London tarehe 5 Oktoba 1963. Barua zote mbilizilikubaliyana juu ya mambo matano yafuatayo:
1) Uhuru wa kuabudu wa watu wadini zote katika sehemu hiyo utalindwa kwa mujibu wa dini zao; na khasa waleraia wa Sultani na vizazi vyao, ambao ni wa dini ya Kiislamu, watahakikishiwauhuru wao wa kuabudu katika nyakati zote na hifadhi za nyumba na sehemu zote zadini yao.
2) Uwezo wa Kadhi Mkuu na Makadhiwengine wote kuhukumu kwa sharia ya Kiislamu utahifadhiwa kufuatana na shariaya Kiislamu katika kesi zote za ndoa, talaka na mirathi.
3) Katika zile sehemu ambazowakaazi wake wengi ni Waislamu, watawekwa, kila inapowezekana, Maafisa Utawala(Mabwana Shauri) Waislamu.
4) Watoto wa Kiislamu, kwa kadriinavyowezekana watasomeshwa lugha ya Kiarabu katika kudumisha dini yao ya Kiislamu kwa vile lugha hii ndiyo lugha ya dini yao. Ule msaada wa fedhaunaotolewa kuzisaidia skuli za msingi za Kiislamu katika hilo jimbo la Mkoa wa Pwani utaendelea.Hautakatwa.
5) Umilikaji wa ardhi kutokana namikataba iliyokwisha kusajiliwa utatambulikana na kukubalika wakati wote.Mwenendo huohuo utaendelea na kuhifadhiwa katika kusajili mikataba mipya yakumiliki ardhi isipokuwa tu pale itakapokuwa ni lazima kuchukua ardhi kwamasilahi na faida ya umma; lakini papo hapo wale wenye ardhi zao watabidikulipwa fedha.6
Kwa mujibu wa Sheikh Abdillahi,makubaliano hayo baina ya Serikali ya Zanzibarna Serikali ya Kenyahayakutimizwa na amethibitisha namna nguvu za umma zilivyoporwa na umuhimu wakujenga muamko wa kuelewa badala ya muamko wa hamasa. Mfano mkubwa ambaoameutowa Sheikh Abdillahi am-bao ni kinyume na makubaliano waliyotiya sahihiMawaziri Wakuu wa Zanzibar na wa Kenya, ni kunyanganywa Waislam, wa makabilayote, Taasisi muhimu sana ambayo ikijulikana kwa jina maarufu la MombasaInsititute of Muslim Education (MIOME) ambayo ilikuwa ni:
baraka kubwa kwa Waislam waAfrika Mashariki. Hapa ndipo mustakbal wa vizazi vya Waislam vinapewamafundisho katika masomo ya ufundi chini ya Maprofesa mabingwa ambaowameajiriwa na Serikali kutoka Ulaya. Sir Phillip Mitchell ambaye alikuwa niGavana na sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Waendeshaji wa Taasisi alikuwa ndiyonguvu ya usukumaji wa Taasisi [MIOME]. Mtukufu Sultan wa Zanzibar alitowamchango wa Shs. 2,000,000/-kutoka mfuko wa Colonial Welfare Fund, Mtukufu AgaKhan alichangiya Shs. 2,000,000/-: Mtukufu Sheikh Mkuu wa jamii ya Kibohoraamechangiya Shs. 1,000,000/-; na Sheikh Khamis Mohammed bin Juma [El Mutwaji]amekodisha ekari 34 na nusu za ardhi nzuri na kwa muda mrefu kwa matumizi yaTaasisi, na kwa bei khafifu kwa kila mwaka.7
Mbali ya Muslim Teachers’Training College iliyokuwepo Kibuli, Kampala, Uganda, Khamisi Sekondari yaMombasa, Muslim School ya Soroti, ya Jinja, na kadhalika.
Iliyovunja rekodi zote na ambayomarehemu Sheikh Ali Muhsin akiamini kuwa ndiyo moja kati ya sababu zakupinduliwa Zanzibar,ilikuwa ni fikra na mipango ya kuanzisha Chuo Kikuu Cha Kiislam cha AfrikaMashariki na Kati. Kwa mujibu wa Sheikh Ali Muhsin, Chuo hicho kilikuwa nalengo la kuwafundisha Waislam kutoka sehemu zote za Afrika Mashariki na Kati. Mwandishiwa ramani wa Chuo hicho alikuwepo Zanzibarmapinduzi yalipotokeya na alisaidiwa kuondoka na Bwana Ahmed Omar Jahadhmy.Wamasri waliishauri serikali ya Zanzibarwasubiri mpaka watakapokuwa na wanafunzi wa kutosha ambao wataweza kufundishwakwenye Chuo hicho. Fikra iliyoona mbali kwa wakati huo ni hii ambayo leoinaitwa Open University. Redio na televisheni vilikuwa viwe ndiyo vyomboviwiili vikubwa vya kufundishiya kote Afrika Mashariki na Kati. Majaribio yakwanza yalifanywa kabla ya mapinduzi lakini yalifeli.8 Baada ya kuvunjwa kwa EastAfrican Muslim Welfare Society ambazo khabari zake zinapatikana kwa urefukwenye kitabu cha Kiswahili cha Bwana Mohamed Said cha Maisha na Nyakati zaAbdulwahid Sykes, taasisi na mali zake zote zikataifishwa nabadala yake pakaundwa BAKWATA Tanzania, SUPKEM Kenya na UMSC Uganda. Hali yaWaislam chini ya utawala wa Kiingereza ilikuwa ni ya kuridhisha zaidi kulikohali waliyokuwa nayo baada ya kupatikana uhuru Tanganyika,Kenya na hata Uganda.
Waingereza Walijuwa Nini KuhusuMapinduzi?
Ukiangaliya kwa makini utakujakuona kuwa walikuwepo Waingereza na mamishionari ambao walikuwa hawana chukidhidi ya Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu lakini kwa bahati mbaya sauti zaosio zilizokuwa zikisikilizwa na kupewa nafasi. Kwa mfano alikuwepo Dk. GeraldBroomfield ambaye alikuwa ni mmishionari wa Kianglikani aliyekuwa na uzowefumkubwa Zanzibar.Dk. Broomfield alinukuliwa na Arab Association ya Zanzibar kutoka kitabu chakeColourConflict in Africa kwa maneno yake yafuatayo:
Afrika iliyobakiya ina jambo lakujifunza kutoka Zanzibar…Zanzibar inaonyesha uwezekano wa kuwepo amanina kuhishimiana baina ya makabila. Huenda likawa ni jambo zuri kwa roho zetukukumbuka [Zanzibar]inafanya hivyo kwa sababu Sultan wa Kiarabu ndiye mkubwa wa Dola.9
Hilo halistaajabishi kwa sababu Ukristouliingiya Zanzibarna bara kwa kupewa hishma na Masultani waliokuwa ni Waarabu na Waislamu. LakiniMuingereza mtawala alipoona kuwa Ufalme umegeuka na kuiunga mkono siasa yakizalendo ya chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) ambayo ilikuwa karibusana na siasa ya uzalendo wa Kiarabu (Pan-Arabism au Arab Nationalism) wa GamalAbdel Nasser wa Misri, akaamua kuwatupa mkono ZNP-ZPPP na kuubwaga uhuru waZanzibar ambao ulikuwa hauna salama kwa Waingereza au kwa Mwalimu Nyerere kwasababu, na kama alivyoelezeya Sheikh Abdillahi:
Zanzibar ilikuwa ni nchi pekee katika Afrika nzima ambayo isingelihitajiya Mzunguhata mmoja. Zanzibarilikuwa ina watu wa kuendesha nchi na kuwaazima majirani kuendesha nchi zao.10
Sababu kubwa ya Wazanzibari wenyeasili ya Kiarabu kuwageuka watawala wa Kiingereza na watawala hao kupangakuwakomowa Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu, kulianza kwa kupigwa mabomuMisri na Muingereza mwaka 1956.11 Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu walihisikuwa Uingereza haiaminiki na kuwa ilikuwa dhidi ya Waarabu. Hisia hiiilisababisha kudai uhuru kamili bila ya kungojea maendeleo zaidi ya baadae.
Mwisho wa mivutano Muingerezaalikataa kuisaidiya serikali ya Zanzibarilipopinduliwa tarehe 12 Januari 1964 na sababu kubwa iliyowafanya kukataa niimani yao kuwa Mapinduzi ya Zanzibaryalikuwa ni suala la ndani ya Zanzibar na kuwahakukuwa na mkono au uvamizi kutoka nje ya Zanzibar. Kwa upande wa Tanganyika Muingerezaaliamuwa kuzuwiya fujo na kumrejesha kitini Mwalimu Nyerere pale jeshi laTanganyika lilipoasi tarehe 20 Januari 1964 na Nyerere akakimbilia mafichonisiku tisa tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar.12 Viongozi wa Serikali yaTanganyika haraka walikwenda kuomba msaada kutoka kwa wakubwa wa Kiingereza.Anaelezeya Brigadier Douglas:
Kambona, akifuatana na [Paul]Bomani, Waziri wa Fedha, akionekana ana jambo ameficha, na ana khofu zaidikuliko kabla, walikuja nyumbani kwangu na barua kutoka kwa Naibu Raisi Kawawailosema: Nimeelekezwa na Raisi wa Jamhuri ya Tanganyika kuiletea ombi la msaadawa kijeshi serikali ya Kiingereza ili utuwezeshe kuweka sheria na amani ndaniya nchi.13
Mara nyingi uasi wa jeshi laTanganyika umekuwa ukihusishwa na mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa wanajeshi waTanganyika, Kenya na Uganda waliingiwa moyo wa kuasi kutokana na kufaulu kwaMapinduzi ya Zanzibar ingawa hakukuwa na uhusiano wowote baina ya matukio hayomawili. Uamuzi huu unatokana na kukosekana kuyafahamu Mapinduzi ya Zanzibar kwanza, na pili, kukosekana huko kufahamika kwamapinduzi ya Zanzibar kumeondowa hoja yakufanywa utafiti wa mahusiano baina ya mapinduzi na uasi wa kijeshi wa Tanganyika.
Suala moja muhimu ambalolinavutiya hoja ya uhusiano baina ya mapinduzi ya Zanzibarna uasi wa kijeshi wa Afrika Mashariki ni suala la kukamatwa kwa viongozi wavyama vya wafanyakazi baada ya kutokeya uasi huo Tanganyika. Tarehe 29 Januari 1964Balozi wa Kiingereza kwa niaba, alipeleka ujumbe wa telegram kwa CommonwealthRelations Office, London, uliopitiyaUbalozi wa Kiingereza Kampala, Nairobi,Aden naWashington:
Matokeo ya kuasi kwa jeshi la Tanganyika ni kundi kubwa la viongozi wa vyamavya wafanyakazi kukamatwa Jumapili usiku Tanganyikanzima pamoja na takriban viongozi wote wa chama cha Shirikisho la Wafanyakaziwa Tanganyika(Tanganyika Federation of Labour). Wote walipelekwa kwenye vituo vya polisi kwakuhojiwa na baadhi yaobaadaye waliwachiwa huru. Rais [Nyerere] kwenye hotuba yake ya redio ya janausiku aliligusiya suala hili na aliongeza kwa kusema kuwa Mkuu wa Wilaya mmojapia amekamatwa.
Nyerere alitamka kwenye hotubahiyo ya redio kuwa watu hawa, wa vyama vya wafanyakazi, walikuwa wamekula njamana viongozi wa uasi wa kijeshi “kusababisha mtafuruku zaidi.” Kulikuwa na uvumimwingi wiki iliyopita kuwa vyama vya wafanyakazi vilikuwa vinapanga mgomo wajumla au angalau mgomo wa wafanyakazi wa gatini na wa reli. Pia inaaminiwa kuwaviongozi kadhaa wa vyama vya wafanyakazi walikuwa wakipitisha wakati wao mwingikwenye kambi ya kijeshi ya Colito.14
Msomaji anaombwa baadayeaunganishe mchango wa vyama vya wafanyakazi katika mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 na uasi wa jeshi la Tanganyika watarehe 20 Januari 1964.
Waingereza hawakuwacha kuuhusishauasi wa jeshi la Tanganyikana mchango wa Oscar Kambona ambaye wakati huo alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Njena Ulinzi. Walimuandikiya makala kwenye ukurasa wa nyuma wa gazeti la DailyTelegraph la tarehe 22 Januari 1964 ambayo ilimuudhi sana Kambona. Balozi wa Kiiengerezaaliyekuwepo Dar es Salaam alielezeya kwenyebarua yake aliyompelekea Bwana W.G. Lamarque wa Commonwealth RelationsOffice, Downing Street, London, kuwa “Stephen Milesalipokutana na Rais [Nyerere] wiki iliyopita waligusiya kuwa Kambona alikuwakiongozi wa uasi wa kijeshi, na Rais, kamaunavyojuwa, alimwambiya Oscar kuwa ‘Masikini Oscar, maisha yeye ndiye mwenyekulaumiwa.’ Kwa kusema kweli, Oscar alikasirishwa sana alipozisikiya habari hizo na akaanguwakilio na ikabidi apewe siku moja nzima ya mapumziko.”15
Waingereza walimtiliya shaka sana Kambona kuwa alikuwa amehusika na uasi wa jeshi la Tanganyika kwakuzingatiya kuwa katika siku mbili za kwanza za uasi, Kambona alikuwaakitangaza kwenye redio kila baada ya nusu saa na kuwa alikuwa tayari achukuwekhatamu za serikali na ajitangaze kuwa ni Rais lakini aliogopa dakika zamwisho. Pia walilalama kwa kusema “Lazima iulizwe kwanini ulinzi wa ndani wa Tanganyika dhidi ya tukio kamala uasi wa jeshi ukawa dhaifu namna hii. Hapana shaka kukosekana kwa taarifakutoka vyombo vya usalama kuipa serikali kumetokana na Kambona na [Job] Lusindekulibomowa Tawi la Usalama na badala yake kuwaweka watu wa T.A.N.U.aliowachaguwa Kambona.”16 Licha ya kuwa hawakuwa na taarifa za kiusalamawatawala wa Kiingereza waliamuwa kupeleka jeshi la Makamandoo kurudisha amanina utulivu Tanganyikana kumrudisha kitini Mwalimu Nyerere.
Na Zanzibar ikapinduliwa, mauwajiya halaiki yakafanywa, na Bwana Adrian Forsyth-Thompson aliyekuwa PermanentSecretary katika ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Mohammed Shamte akaondokaZanzibar tarehe 8 Februari 1964, na alitarajiwa kuondoka Nairobi kuelekeya CapeTown, Afrika Kusini, tarehe 11 Februari 1964. Baba yake Adrianalikuwa ni ofisa katika serikali ya kikoloni ya Kiingereza na alistaafu CapeTown. Adrian aliondoka Cape Town tarehe 18 Machi kwenda kwenye kazi yake mpya katika visiwa vyaSeychelles.
Forsyth-Thompson alikuwa ni ofisawa usalama kwenye ofisi ya Balozi wa Kiingereza Zanzibar na punde tu kabla yamapinduzi alikabidhiwa kazi na Katibu Mkuu wa Kiingereza, Bwana Mervyn ViceSmithyman, katika ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Mohammed Shamte kuleta mabadilikokatika vyombo vya usalama vya Zanzibar.Alipokuwapo Nairobi na tayari kuondoka kwenda Cape Town, Forsyth-Thompsonalitowa ripoti muhimu ambayo ilipelekwa Commonwealth Relations Office,London kwa njia ya telegram na kopi zikapelekwa ubalozi wa Kiingereza Dar esSalaam, Aden, Kampala, Washington na Cape Town. Ujumbe huo ulikuwa ni mfupiukiufananisha na ripoti yake yenye kurasa nane aliyoiandika alipokuwa Nairobi tarehe 10Februari 1964.
Kwenye ripoti fupi aliyoitowa Nairobi na iliyopelekwa London na Washington, Forsyth-Thompsonaliziwasilisha nukta tano lakini hapa tutainukuu nukta ya kwanza na nukta yanne:
1) Hakuna (rudia hakuna) ushahidiwa mkono kutoka nje katika mapinduzi ambayo yalikuwa ni mapinduzi yaAfro-Shirazi Youth League dhidi ya siasa ya Kiarabu ya Serikali iliyokuwepo, namapinduzi yalifanywa katika kipindi ambacho viongozi wa ASYL na washabiki waowakiamini patatokeya ukamataji wa viongozi wakati wowote. Babu alichupiya, naKarume (? Alichaguliwa) na wanamapinduzi kuwa ndiye kiongozi anayejulikana naOkello alichomoza tu.
4) Kwa mtizamo wa mbali mustakbalwa Zanzibar umo katika uhusiano wa karibu namaeneo ya bara ikiwa ndani ya Shirikisho au kuunganishwa na Tanganyika.Hili litafanyika kwa urahisi ikiwa Tanganyikaau Kenyawatakuwa tayari kupeleka vikosi vya polisi (kwa mfano kikosi cha huduma)kutokana na ombi la Karume ambaye atakubali kutokana na hali ya mambo ilivyoikiwa Watanganyika na Wakenya watampa ishara kuwa wako tayari.17
Kwenye ripoti yake ya kurasanane, Forsyth-Thompson anaelezeya kuwa:
Umma Party na viongozi wa ASPwenye mitizamo isiyo mikali hawakujuwa chochote [kuhusu mapinduzi]. SalehSaadalla labda akijuwa…Alkhamisi tarehe 9 [ASYL] walisikiya kuwa mzigo wa meliwa silaha kutoka Algeriaulikuwa utaletwa na Serikali…Hadithi za silaha kutoka Algeriazilikuwa zimezagaa kwenye wiki baada ya mapinduzi: na kwa hakika ulikuwa niupuuzi mtupu.18
Kuhusu mapinduzi yenyewe,anaelezeya Forsyth-Thompson, “yalipangwa na kutekelezwa ndani ya muda mfupi nahii ni dalili ya kukosekana kabisa taarifa zozote kutoka kitengo cha usalama(Special Branch) kuwa kulikuwa na mpango. Kwa muda mrefu kulikuwa na mazungumzoya kufanya fujo, lakini hakukuwa na pendekezo la mpango wa kuipinduwaSerikali kwa kutumiya nguvu.”19
Kamati ya Ukombozi wa Afrika
Mkutano wa nchi huru za Kiafrikauliofanyika Addis Ababamwezi wa Mei 1963 uliunda Kamati ya Ukombozi wa nchi tisa yenye makao makuu Dares Salaam. Nchi zilizounda kamati hiyo zilikuwa Tanganyika,Nigeria, Uganda, Algeria,Umoja wa Jamhuri ya Kiarabu (U.A.R.), Guinea,Senegal, Ethiopia naKongo. Ghanahaikuwemo.
Nyerere hakupendeleya makao makuuya Kamati ya Ukombozi ichukuliwe na Ghana,U.A.R. au Algeria.“Alikhofiya kuwa kati ya nchi hizo Kamati ingelitumiliwa na Rais wa Dolakujijengeya sifa, na mtizamo wa kamati ungelikuwa juu ya utumiaji nguvu badalaya shinikizo la amani.”20
Baada ya uchaguzi wa mwisho waZanzibar wa kabla ya mapinduzi wa tarehe 8 Julai 1963, Mwalimu Nyerere alifanyaziara ya Marekani na alionana na Rais John F. Kennedy, na Katibu Mkuu wa Umojawa Mataifa U Thant. Pia aliitembeleya nchi ya Canada kwa muda mfupi na alikuwa namazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bwana Lester Pearson. Tarehe 21–25Julai alikuwa mgeni wa Serikali ya Uingereza. Mwalimu na ujumbe wake uliondoka London siku ya Alkhamisi tarehe 25 Julai kuelekeya Algiers, mji mkuu wa Algeria.
Katika msafara wa Rais Nyererewalikuwemo:
Rais Nyerere
Bwana Oscar Kambona, Waziri waMambo ya Nchi za Nje na Ulinzi
Bwana I. M. Bhoke Munanka (WaziriMdogo, Ofisi ya Makamo wa Rais)
Bwana A. B. C. Danieli (KatibuMsaidizi, Mambo ya Nje)
Bwana G. Rockey (Katibu waHabari)
Bwana F. Sangu (A.D.C.)
Bwana P. Mwinbo (Mkuu wa MaofisaWafanyakazi)
Bwana J. M. Simba (Katibu Khasawa Rais)
Bwana U. Nyondo (Ofisa Mfanyakazi wa Rais)
Bwana K. Kondo (Ofisa Mfanyakaziwa Bwana Kambona)
Ziara rasmi ya Rais Nyerere namsafara wake nchini Algeriailikuwa kuanziya tarehe 25 mpaka tarehe 28 Julai. Inavyoonesha Ubalozi waKiingereza mjini Algiers hakuambuliya kituchochote cha maana kati ya mazungumzo ya Rais Nyerere na Ahmed Ben Bella,Waziri Mkuu wa Algeriana baadaye Rais wa nchi hiyo.
Katika mwezi huohuo wa Julai 1963Waingereza walikuwa wameshazipata habari kutoka jeshi la Tanganyika kuwa kulikuwa na silaha zikitarajiwakutoka Algeria.Baina ya mwezi wa Agosti na Septemba 1963 listi ya silaha ilionekana Wizara yaUlinzi. Halafu kimya mpaka wiki ya kwanza ya Januari 1964.21
Tarehe 2 Januari 1964, meliiliyopewa jina la mwanafalsa maarufu duniani wa historia, MV Ibn Khaldun kutokanchi ya Kiarabu ya Afrika ya Kaskazini ya Algeria,ilitia nanga Dar es Salaam huku ikibeba shehenaya silaha zilokusudiwa kupelekwa Msumbiji na kwa ajili ya mapinduzi ya Zanzibar. MV IbnKhaldunhaikuwa Sultana iliotiya nanga New York Alkhamisi, tarehe30 Aprili mwaka 1840 na iliyobeba ujumbe wa amani na biashara kutoka Zanzibar kwa SultanSayyid Said bin Sultan.
Meli ya MV Ibn Khaldun ilikuwepoDar es Salaam kwa siku nane, kuanziya tarehe 2 Januari 1964 na iliondoka tarehe9 Januari 1964. Ilipowasili mara ya kwanza meli hiyo “ilikaa nje ya bandari ya Dar es Salaam kwa muda wamasaa arubaini na nane. Kutokana na kuhojiwa kwa maofisa wa Kiafrikawaliohusika na upakuwaji wa mizigo ya meli ilikuwa dhahiri baadhi ya mizigoiliondolewa na inawezekana sanakuwa baadhi yake iliondolewa kabla ya meli kufunga gati.”22 Rais Nyererealiongozana na Bwana Djoudi aliyekuwa Charge d’Affaires katika Ubaloziwa Algeria Tanganyika katika kuikaguwa meli hiyo. Djoudi pia alikuwa mhusika wamafunzo ya kijeshi wa Kamati ya Ukombozi wa nchi tisa za Kiafrika. Kijana mdogomwenye umri wa miaka 24 aitwaye Racchid Ben-Yelles alikuwa Kepteni wa meli hiyoya MV Ibn Khaldun.
Kepteni Ben-Yelles alitowamaelezo kuwa meli hiyo ambayo alichukuwa dhamana ya kuiyendesha miezi mitatunyuma ilikuwa kwa kawaida yake ikifanya kazi kwenye Bahari ya Mediterranean.Mzigo wa kawaida wa meli hiyo ulikuwa ni ulevi wa zabibu na meli hiyo ambayoikimilikiwa na Serikali ilikuwa na matenki yenye uwezo wa kubeba tani 2,000.Meli ilipoondoka, Rais Nyerere aliwapungiya mkono kepteni na wafanyakazi wakena kuwaombeya safari njema. Wakati inaondoka meli hiyo ilikuwa imebeba shehenaya tani 80 za kahawa na tani 100 za mbao kutoka Tanganyika na ilielekeya Tangakuongeza mizigo zaidi.23
Kwa mujibu wa ripoti ambayohaiyoneshi imetoka kwa nani na inakwenda kwa nani, Serikali ya Tanganyikailiwalipa Waalgeria “thamani ya pauni za Kiingereza 260,000 za kahawa na bidhaanyengine.”24 Wapi pesa hizo zilitoka bado ni suala la michirizi yakekufuatiliwa. La muhimu ni kahawa na mbao yalikuwa ni malipo kwa ajili ya silahazilizoletwa kutoka Algeriana meli ya Ibn Khaldun. Kwa amri ya Oscar Kambona, kazi ya upakuwajiwa mizigo ya silaha hizo alipewa Kepteni Nyerenda na aliamrishwa mzigo wote wasilaha auweke kunako ghala za P.W.D. (Public Works Department).25
Huo ulikuwa ni wakati wauanzishaji wa harakati za ukombozi wa Msumbiji na baadaye kuanzishwa kambi zakuwapa mafunzo wapiganiya uhuru wa Msumbiji Tanganyika. Oscar Kambonaaliwababaisha waandishi wa habari kwa kuwaambiya kuwa silaha kutoka Algeriazilikuwa kwa ajili ya Tanganyika Rifles lakini Waingereza walipotakataarifa zaidi kutoka kwake aliwajibu kuwa “…ni za Tanganyika Rifles isipokuwamaboxi yaliopigwa krosi nyeusi. Maboxi haya yanatakiwa yawekwe karibu na mlangowa ghala ili yaweze kuondolewa kwa haraka. Pia alisema kuwa maboxi hayoyasifunguliwe. Tuliyafunguwa baadhi yake…Zanzibarilitokeya Jumapili iliyofuatiliya, tarehe 12 Januari na maboxi yale badoyalikuwepo kunako ghala. Baada ya hapo yakawa hayana umuhimu wowote.”26