mwanazuoni

MBUNGE WA JIMBO LA MASASI MHE: DR RASHID CHUACHUA ATEKELEZA VIPAUMBELE VYAKE ALIVYOKUWA AMEAHIDI KWENYE KAMPENI ZAKE.

Katika harakati zangu za kampeni niliorodhesha vipaumbele vyangu wakati wote wa utumishi wangu wa ubunge kama Dira ya miaka mitano katika ubunge wangu.

Tathmini yangu ya mwaka mmoja sasa.
Maeneo niliyoyapitia katika dira yangu ni yafuatayo:-

1. Maeneo niliyofanikiwa kwa 100%

a) Kuondoa vizuizi barabarani katika jimbo langu.

b) Bei ya mazao, kuboresha bei ya korosho niliahidi kusimamia uboreshaji wa mfumo nasi kuondoa na nilisimamia kikamilifu japo zipo changamoto zilizojitokeza nazo nitazisimamia ili msimu ujao yasijitokeze.

c) Ili ni jambo ambalo ilinaendelea kutekelezwa tu lipo tokea nyuma.

2. Yaliyotekelezwa kwa 60%

a) Elimu safari hii tumeboresha baadhi ya miundo mbinu ya shule kwa kutengeneza madawati na kuwagawia Madawati yaliyotolewa na ofisi ya mbunge kutokea ofisi ya rais na kufanya kutokuwa na upungufu wa madawati katika shule zilizo katika jimbo langu.

Lakini pia katika mfuko wa jimbo tulitoa fedha kwa baadhi ya shule ili wakamilishe baadhi ya huduma. Vilevile niliomba fedha za mradi wa madarasa katika shule mbili Mkuti na Mtandi ili tupate madarasa nane nane mapya na Waziri wa elimu kupitia programme for result walitupatia Milioni 192 kwa kila shule hizo na madarasa yamejengwa nilipigania pega kwa pega kuakikisha tunapata kwa wakati.

b) Maji tumekamilisha miradi miwili wa Chisengu na Mwenge na tumemalizia ule tulioukuta wa Temeke hii tayari inatoka maji, pia tuko mbioni kuanza mradi mkubwa wa maji katika kata tano, Mwenge Mtapika, Sululu, Marika, Mumbaka na Matawale.

c) Afya katika ili nilianza na huduma ya uzazi kuwapatia vifaa vya kujifungulia bure kwa hisani ya Mbunge kwa wanaotokea kwenye jimbo langu pia nilitoa wito kwa Wanamatawale kuandaa eneo kwaajili ya Zahanati na niliwapatia fedha kwaajili ya cement za kuanza kufyatua tofari, pia tuko mbioni kuanza kufyatua tofari kwaajili ya vituo vitatu vya afya.

d) Ushirika, katika ushirika tulishaanza reform kwa baadhi ya vyama kama Mkalamani na Matawale Amcos pia tuna baadhi ya vyama tumevipeleka Mahakamani ni kusudi langu kufanya ushirika Mpya kwenye jimbo langu na unaosimamia usawa na haki kwa wakulima, pia nimepigana kumuondoa mrajisi wa Taifa na Mkoa kutokana na kushindwa kuwawajibisha viongozi wa ushirika katika jimbo langu, Masasi mpya ushirika mpya ndio lengo langu.

e) Ili pia kwa nafasi yangu tayari kuna baadhi ya taasisi nimezichukulia hatua ikiwemo vyama vya msingi na nilitoa namba yangu kuwa yoyote atakayeombwa rushwa tuwasiliane ili tutokomeze rushwa katika jimbo letu. Niseme suala la rushwa ni letu sote tupambane nalo.

f) Ajira, tayari ajira katika Halmashauri yetu tumeajiri vijana wa kutukusanyia ushuru takribani 15, watendaji wapya takriba 8, na ajira binafsi zimezidi kuongezea kutoka 35% hadi kufikia 65%. Kwenye biashara, bodaboda, na kilimo.

g) kilimo katika kilimo tumetoa msimu huu Sulfa ya ruzuku kwa Tsh 14000 tu kupitia vyama vyao vya Msingi, pia tumeandaa mbolea ya ruzuku kwa wakulima ili kuboresha mazao yetu.

3. Maeneo yenye changamoto katika utekelezaji.
a)Viwanda ni changamoto katika mazingira yetu.

Hivyo nawaomba Wanamasasi tuendelee kushikamana na kushirikiana ili tuendelee kusukuma gurudumu la Maendeleo.


Share on Google Plus

. Mtani

Mshana is Tanzanian blogger who writes different news without bias, He provides social, political and sports as well as Entertainment news happening in all parts around the World."STAY ME ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.."
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment