Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anasema kuwa hakupenda kuondoka Chelsea ''kwa machungu' na kwamba amekuwa akiipenda klabu hiyo.
Klabu ya Atletico Madrid imefanya makubaliano na Chelsea ya kumrudisha mshambuliaji huyo ,28, katika klabu hiyo ya Uhispania.
Costa hajaichezea klabu hiyo msimu huu na ametumikia kipindi kirefu cha mwezi Agosti akiwa Brazil alikozaliwa.
''Sitaondoka bila kuishukuru Chelsea, ambapo nilifurahia kuwepo kuichezea timu kubwa'', alisema Costa baada ya kuwasili Madrid. ''Atletico ndio nyumbani kwangu''.
Uhamisho huo ambao utakamilishwa mnamo mwezi Januari unashirikisha makubaliano ya kibinafsi.
Atletico imesema kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 28 ambaye aliondoka klabu hiyo na kujiunga na Chelsea 2014 atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku chache zijazo.
0 comments:
Post a Comment